Katika kuhamasisha uandishi wa maudhui yenye tija mtandaoni na kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama Asasi ya Jamii Forums imezindua awamu ya pili ya shindano la " Stories of Change" litakaloanza Julai 15, 2022 na kumalizika Septemba 14, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Julai 13,2022 Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Maxence Melo amesema kuwa uzinduzi wa awamu yapili unakuja kutokana na mafanikio yaliyopatika katika awamu ya kwanza ya shindano hilo .
"Jamii Forums ikishirikiana na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa umma , Chuo kikuu cha Dar es Salaam SJMC na muungano wa Klabu za Waandishi wa habari ( UTPC) imeaandaa awamu ya pili ya shindano la" Stories of Change " amesema Maxence
Ameongeza kuwa shindano hilo linalenga kuongeza maudhui bora hususani ya lugha ya Kiswahili kwaajili ya vizazi vya na baadae.
" Shindano linalenga kuhamasisha ushiriki wa raia yakiwemo makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini" amesema .
Kuhusu vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hilo Maxence amebainisha kuwa mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Biashara/ Uchumi , Afya, Utawala Bora, Demokrasia , Kilimo, Sayansi na Teknolojia ambalo litaandikwa kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno yasiyozidi 800-1000 na kuliweka andiko lake katika Jukwaa la Jamii Forum's.
Akizungumzia zawadi kwa washindi emesema amesema mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5 , Mshindi wa Pili Milioni 3, wa tatu Milioni 2, wa 4 Milioni 1 na watano ni shilingi laki 5 huku mshindi wa sita mpaka kumi watapata Shilingi laki tatu kila mmoja na mshindi wa kumi mpaka Ishirini watapata Shilingi laki moja kila mmoja.
Amesema washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha ( thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).
Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Bw.Maxence Melo akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya shindano la ‘Stories of Change’ Katika Ofisi za Jamii Forum’s Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 13, 2022
Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Bw.Maxence Melo akipata picha ya pamoja na mhadhiri chuo kikuu Cha Dar es salaam shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano wa umma SJMC Bw.Abdallah Katunzi katika uzinduzi wa awamu ya pili wa shindano la 'stories of change' katika ofisi za Jamii forum
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...