CEO Roundtable Tanzania (CEOrt) imefanya mkutano kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Mkutano huu ni sehemu ya shughuli za kila mwezi za shirika hilo ili kuwezesha majadiliano juu ya masuala muhimu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania
Kufuatia changamoto zilizotokana na majanga ya kimataifa, ukuaji wa kiuchumi uliathirika kwa nchi nyingi, na sasa unaanza kurudi kwenye mstari. Taasisi na sekta mbalimbali zina jukumu muhimu katika kusaidia juhudi hizi za kufufua uchumi, na zimejitolea kuisaidia Serikali katika kufikia malengo ya maendeleo. Kama sehemu ya madhumuni ya shirika kukuza ukuaji na ustawi, CEOrt ina furaha kumkaribisha Dkt. Patricia N. Laverley - Mwakilishi wa Nchi, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) - Tanzania kutoa hotuba kuu kuhusu "Kuendesha Ufufuo wa Kiuchumi wa Afrika."

CEO Roundtable inatarajia kujifunza mengi kutoka kwa Dkt. Laverley, pamoja na kuzungumzia jinsi Sekta Binafsi inaweza kuunga mkono juhudi za Tanzania za kukuza ukuaji wa kasi na kuleta maendeleo ambayo ni endelevu.
Kuhusu CEO Roundtable - Tanzania Shirika linawakilisha Wakurugenzi Wakuu kutoka kampuni zaidi ya 160 zinazoongoza nchini Tanzania kutoka sekta mbalimbali za uchumi kwa madhumuni ya pamoja ya kuongeza matokeo katika uongozi na ustawi endelevu wa jamii na uchumi wa nchi. Kwa pamoja, wanachama wa CEOrt huchangia katika uchumi wa Tanzania kupitia ukusanyaji wa kodi, ajira, kujenga uwezo, kuhamisha teknolojia na kuongeza ujuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...