.jpeg)
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KAMPUNI ya Sukari ya Kilombero imetoa rai kwa wakulima wa miwa nchini kuhakikisha wanatumia fursa ya upanuzi wa kiwanda hicho kwa kuongeza mashamba ili kupunguza uhaba sukari nchini Tanzania huku ikieleza mkakati uliopo ni kuzalisha sukari tani zaidi ya 271 kwa mwaka badala ya tani 130,000 zinazozalishwa sasa.
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Sukari Kilombero Fimbo Nutallah ameeleza hayo alipokuwa kwenye banda la Kilombero kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam ambapo ametumia kuelezea mipango ya Kampuni hiyo katika kuendelea kuzalisha sukari nchini
"Kwa Sasa Kampuni yetu kutokana na kiwanda tulichonacho tunazalisha tani 130,000 kwa mwaka lakini baada ya kujengwa kwa kiwanda kingine kipya basi tutakuwa tunazalisha zaidi ya tani 271,000 kwa mwaka.
"Kampuni tunaamini ujenzi wa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kufungua fursa kwa wakulima wa miwa kuwa na uhakika wa soko maaana uzalishaji ukiongezeka mahitaji ya upatikanaji miwa nao utaongezeka,wakulima waongeze mashamba na kulima zaidi,"amesema.
Aidha amesema uchache wa viwanda vya sukari uliopo nchini kwa namna moja au nyingine unachangia kuongezeka kwa uhaba wa bidhaa hiyo lakini hiyo ni fursa kwa wakulima kuongeza mashamba ya kilimo cha miwa.
Amesisitiza upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kuongeza ukuaji wa uchumi kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho kwani baada ujenzi kukamilika idadi ya watumishi nayo itaongezeka na wakati huo huo biashara nyingine zitafunguka pembezoni mwa kiwanda hicho.
Wakati huo huo katika maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kilombero, Guy Williams na Mkurugenzi mkuu wa Biashara Ilovo Afrika, Andre Lube wamepata nafasi ya kutembelea banda hilo na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mipango yao katika kuongeza uzalishaji ili kukabiliana na uhaba uliopo.
Hata hivyo kwa mujibu wa maofisa wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero wamesema wataendelea kupatikana kwenye maonesho hayo ya Saba Saba ili kuendelea kutoa elimu kuhusu uzalishaji wa sukari pamoja na ubora wa bidhaa hiyo.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la Kilombero wamepata nafasi ya kuona bidhaa zinazozalishwa na Kampuni hiyo nchini Tanzania sambamba na bei zake halisi na kwamba bei zao zimezingatia hitaji la mteja hivyo wanauza kulingana na mahitaji.
Baadhi ya matukio katika picha ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kilombero Suger Guy William akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Biashara Illovo Afrika Andre Lube, walipotembelea banda la Kilombelo Sugar kwenye maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba, wakiwa wanaelekezwa na Mkurugenzi wa Biashara Fimbo Nutallah na Meneja masoko Olympia Fraten.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...