SERIKALI imeonya vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Watoa Huduma vya kujihusisha na vitendo vya udanganyifu ambavyo vinauweka Mfuko huo katika hali ngumu.

Akizungumza na Watoa Huduma wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema vitendo hivyo havikubaliki hata kidogo kwa kuwa vina madhara makubwa katika chombo hicho cha NHIF.

"Ni jukumu letu sisi wote na nyie  watao huduma kuhakikisha mfuko huu unadumu na tunaulinda, ni ukweli usiopingika kuwa bila NHIF uendeshaji wa vituo vyetu utakuwa mgumu sana na hili ndio linaumiza kuwa NHIF tunaitegemea na wakati huo huo tunaihujumu"alisema Mhe. Ummy.

Alisema kuwa asilimia 70 ya mapato ya vituo vingi yanatokana na madai kutoka NHIF hivyo unaweza kuona ni kwa namna gani kila mmoja anapaswa kuulinda Mfuko.

"Natamani  kuona vituo vya kitalaam vikisajiliwa kila siku lakini tatizo kubwa ni uaminifu wa Watumishi wetu ambao wanadiriki hata kufanya vitendo vya kuhamisha wagonjwa kutoka Hospitali za Serikali kwenda binafsi hili halikubali hata kidogo na huu ni udanganyifu " alisema Mhe. Ummy.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa  Umoja wa Wamiliki wa Hospitali Binafsi Dkt. Egina Makwabe aliweka wazi msimamo wa umoja huo kuwa hautetei aina yoyote ya udanganyifu  na inachoelekeza ni utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza katika Mkutano wa watoa huduma za Afya wa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumia wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wenye lengo la kupokea maoni mbalimbali ya kuboresha sekta ya afya nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Kisenga, Millenium Tower, Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Juma Muhimbi  akizungumza katika Mkutano kati ya Waziri wa Afya na watoa huduma za Afya wa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumia kwa wanachama wa NHIF, ulioratibiwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye ukumbi wa Kisenga, Millenium Tower, Dar es salaam.  

 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza katika Mkutano kati ya Waziri wa Afya na watoa huduma za Afya wa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumia kwa wanachama wa NHIF, ulioratibiwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye ukumbi wa Kisenga, Millenium Tower, Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Hospitali Binafsi (APHFTA), Dkt. Egina Makwabe akizungumza katika Mkutano kati ya Waziri wa Afya na watoa huduma za Afya wa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumia kwa wanachama wa NHIF, ulioratibiwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye ukumbi wa Kisenga, Millenium Tower, Dar es salaam.  
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Dkt. Rashid Mfaume akizungumza katika Mkutano kati ya Waziri wa Afya na watoa huduma za Afya wa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumia kwa wanachama wa NHIF, ulioratibiwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye ukumbi wa Kisenga, Millenium Tower, Dar es salaam. 







Sehemu ya watoa huduma za Afya wa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumia wanachama wa NHIF, wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) katika Mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Kisenga, Millenium Tower, Dar es salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...