MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrhaman Kinana ametembelea Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kufurahishwa kwake na jitihada zinazofanywa na Serikali kuweka mazingira mazuri ya wananchi kushiriki shughuli za uchumi.

Akizungumza baada ya kumaliza kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho Kinana amesema amefurahi namna wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi wanavyoshiriki kwa hamasa kubwa na wanavyoonesha shughuli za uzalishaji , viwanda , biashara na uwekezaji.

"Lakini jambo kubwa zaidi ambalo limenifurahisha ni kila mshiriki alivyoweza kuonesha juhudi anazofanya katika kuchangia uchumi wa Taifa letu , maendeleo ya Taifa letu na kwa namna kujaribu kutatua tatizo la ajira kwa vijana lakini kukuza uchumi wa nchi.

"Nimeona kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara kwa kutengeneza viwanda vidogo vidogo vitakavyowezesha wakulima mbalimbali kama vile wa sukari,alizeti na mazao mengine kuwa na viwanda vyao vidogo vidogo na kutengeneza bidhaa katika eneo dogo na kwa idadi ndogo ya watu.

Amesema ameona namna ambavyo kumekuwa na bunifu mbalimbali kutoka kwa washiriki ambao utasaidia watu kujitegemea huku akieleza kwa mazingira na jitihada zinazofanyika kuna uwezekano wa mahitaji mengi kama sukari na mafuta na bidhaa nyingine zikawa zinapatikana hapa hapa nchini.

"Kwa hiyo nawapongeza Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa namna wanavyoweza kuwasaidia vijana wetu kujiari na kuajiriwa na mara nyingi tunataka vijana wajiajiri lakini tusipotengeza fursa za watu kujiajiri, na mazingira ya watu kujiajiri kauli itabaki kuwa kauli bila utekelezaji."








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...