Na Mwamvua Mwinyi,Pwani


MKUU wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge amepokea ng'ombe 500 na mbuzi 1,000 kutoka Taasisi ya IDDEF kutoka nchini UTURUKI na Taasisi ya RAHMAN kwa Ajili ya sadaka ya kuchinja inayoyolewa katika Eid Al Adha.

Lengo la sadaka hiyo Ni kugawiwa katika wilaya zote kwa watu wenye mahitaji maalum ,wajane ,wazee na vituo vya yatima na wenye mahitaji.

Kunenge anasema ,sadaka hiyo Ni sehemu ya ibada kusheherekea sikukuu hiyo kwa waumini wote na wasio waumini wa kiislam.

;"Nchi yetu imeendelea Kuwa na amani ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuondoa kero kwa wananchi na kutoa fursa kwa wananchi kufanya ibada kulingana na dini zao:;.

"Serikali haina dini na ndio maana inashirikiana na Taasisi mbalimbali kufanya na kutekeleza kutoa misaada na kufanya shughuli za kidini;". alifafanua Kunenge.

Amesema pia baadhi ya wafugaji wa Mkoani hapo wameweza kunufaika kupata kipato kwa kuuza ng'ombe na mbuzi

Kunenge anaeleza kwamba ,hakukuwa na mifugo hiyo hivyo Taasisi hiyo imenunua mifugo kutoka kwa wafugaji.

Akikabidhi sadaka hiyo kwa Mkuu wa mkoa huyo , mwakilishi kutoka IDDEF Turky Ahmad Furqan alieleza kuwa ,imekuwa ni sehemu ya tamaduni yao kutoa sadaka kwa waislam na wasio waislam .

Alisema, Jumuiya ya Uturuki katika huduma za ng'ombe Kuna nchi 40 wanazihudumia na zenye umma ambao wenye mahitaji .

"Rais wa Uturuki yupo katika kushirikiana na nchi za Afrika kiuchumi na kimaendeleo na kuwezesha kwenye masuala ya kidini ,Tunamshukuru Rais Samia kutupa nafasi ya kuingia Tanzania na kutoa sadaka hii.."

"Pia tunamshukuru mkuu wa Mkoa kuunga mkono kutoa eneo hili la Machinjioni kuhifadhi mifugo hii na siku ya sikukuu inshallah tutagawa nyama kwa watu kwenye Maeneo mbalimbali ikiwemo misikiti kwa waumini na wananchi."alisisitiza Furqan.

Kwa upande wake ,Mwakilishi BAKWATA Pwani ,Salmin Buda watagawa kwa haki kwa makundi lengwaKwa niaba ya sheikh wa mkoa wa Pwani ambae pia ni Katibu wa Baraza la masheikh mkoa ,Salmin Buda alipokea sadaka hii kutoka mkoa kwa Lengo la kuitoa kwa walengwa.

Buda anaeleza ,watahakikisha wanasimamia kufikia walengwa ili kufanikisha sadaka hii ya kuchinja katika sikukuu ya Eid Al Adha.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...