NA BALTAZAR MASHAKA, Ilemela
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Sahili Geraruma amezindua mradi wa maji wa Mlimawa rada wilayani Ilemela uliojengwa kwa zaidi ya sh.milioni 365.5 nakuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Akizundua mradi huo uliojengwa na mkandarasi mzawa kampuni ya kizalendoya URSINO LTD, Geraruma alisema umetekelezwa kwa ubora wa viwango kulingana na thamani ya fedha za walipa kodi na kuipongeza kwa kazi hiyo nzuri.
“Nimeridhishwa na mradi huu kwa namna ulivyotekelezwa na kampuni ya kizalendo ikiongozwa na wazawa,
imeufanya kwa weledi, umetoa ajira kwa wananchi na wamepata kipato,
umekamilika na utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi waKiseke na
maeneo jirani,”alisema.
Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na
Usafi wa MazingiraJijijni Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard
Msenyele,alisema mradi huo umetekelezwa kutokana na mahitaji ya huduma
ya maji kwa wananchi na sera ya maji ya mwaka 2002,Mpango Mkakati wa Maji
nautekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya
mwaka 2020-2025.
Alisema mradi huo umegharimu sh.365,580,080 kwa
fedha za serikali kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na
Mapambano dhidi ya Uviko -19, umekamilika kwaasilimia 100 utaanufaisha
wakazi 3,600 wa Kiseke, katika Manispaa ya Ilemela.
“Mradi huu
utasaidia upatinakaji wa huduma ya maji katika Kata ya Kiseke, hasa
wakazi nawananchi wanaoishi katika miinuko (mlima wa Rada),utwanufisha
wananchi 3,600 nautaongeza kiwango cha upatikanaji wa maji safi na
salama kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya URSINO Ltd, Mhandisi
Mnandi Mnandialisema kazi iliyotekelezwa katika mradi huo ni kulaza
bomba kuu lakusafirishia maji la urefu wa km 3,kulaza mabomba ya
kuzambazia maji, ujenzi wachemba tatu,usimakaji wa pampu yenye uwezo wa
kuzalisha lita 35,000 za maji kwa saa na ujenzi wa tenki la
kuhifadhiamaji lenye ujazo wa lita 150,000.
“Niishukuru serikali ya
awamu ya sita kwa kutupatia kazi ya kujenga miundombinu yamaji kwa
manufaa ya wananchi wa Kiseke na kuhakikisha inakamilika na kupatahuduma
ya maji safi na salama karibu na makazi yao,”alisema Mhandisi Mnandi na
kuahidi kuendelea kufanya kazi mbalimbali za miradi ya huduma ya jamii
kwa weledi endapo watapewa kazi na serikali.
Aidha Mary Protas,mkazi
wa Kiseke, alisema kukamilika kwa mradihuo wa maji ni faraja kubwa kwa
wananchi wa eneo hilo, kwa sababu walikuwa wakipata adha kubwa yahuduma
ya maji safi na salama kwa wa matumizi mbalimbali, pia walilazimika
kuamka usiku kupanga foleni ili kupata maji.
“Kwa niaba ya
wananchi wa Kata ya Kiseke na mlima wa rada hasa wanawake tunamshukuru
sana Rais Samia SuluhuHassan kwa kusikia kilio chetu na kutujali kasha
akatoa fedha za kujenga mradihuu, tunaahidi kuwsimama naye muda
wote,”alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...