Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini
Asangye Bangu akiwa na wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika
Ligunga Wilaya ya Tunduru alipokutana na wakulima wanaotumia mfumo wa
stakabadhi ghalani katika kijiji cha Ligunga Tunduru.
Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye Bangu akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika Ligunga Wilaya ya Tunduru kuhusiana na mpango wa kuanzisha pensheni ya uzeeni kwa wakulima.
Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye Bangu akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika Ligunga Wilaya ya Tunduru kuhusiana na mpango wa kuanzisha pensheni ya uzeeni kwa wakulima.
WAKULIMA wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wanatarajia kuanza kupata pensheni ya uzeeni.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye
Bangu Akizungumza na vyama vya Ushirika vya Msingi vya Ligunga,Namatili
na Mtetesi katika Wilaya Tunduru,amesema,serikali imedhamiria kuhusisha
Mfumo wa stakabadhi ghalani na pensheni kwa wakulima ili wakulima
waweze kumudu kuendesha maisha yao wanapokuwa wazee.
Amesema
uwezo wa kufanya kazi kwa wakulima wakiwa vijana ni tofauti na
wanapofikisha miaka 60 hivyo wakulima watakaokuwa wanauza kwenye Mfumo
wa stakabadhi ghalani michango yao kidogo kidogo itafanyika kwenye
mfumo ili kujiwekea pensheni uzeeni.
"Nguvu
zinapokuwa zimepungua,mashamba bado unayo hivyo pensheni itawawezesha
wakulima wazee kuendelea kupata fedha za kuwalipa vibarua watakaokuwa
wanawafanyia kazi za kilimo",alisisitiza Bangu.
Hata hivyo amesema pensheni hiyo kwa wakulima itaunganisha na mambo mengine muhimu kwa wazee kama Bima za Afya na mikopo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,serikali ipo katika hatua za awali za kuhakikisha kuwa suala la pensheni kwa wazee linafanikiwa.
Bangu
amebainisha kuwa wataalam watapita kwa wakulima ambao watapenda
kujiunga kwenye mfumo huo ili kutoa elimu ya uelewa kabla ya kuanza
utekelezaji wake.
Amesema licha ya kwamba pensheni
kwa wakulima ni jambo geni lakini litakuwa msaada mkubwa kwa wakulima
na kwamba litaongeza hamasa kwa vijana ambao bado wana nguvu lakini
baada ya miaka kadhaa watafikia uzeeni.
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru TAMCU Musa Manjaule ameutaja mfumo
wa stakabadhi ghalani kuwa una faida nyingi kwa mkulima.
Manjaule
amesema wakulima wa Tunduru walianza kutumia mfumo wa stakabadhi
ghalani tangu msimu wa mwaka 2015/2016 hali inayowawezesha wananchi
kuendelea kupata bei nzuri ya mazao.
Amewataja
mazao ambayo yapo kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani Wilaya ya Tunduru
kuwa ni korosho,ufuta na mbaazi na kwamba wakulima wanafurahia mfumo huo
ambao umeboresha maisha yao kwa sababu wanalipwa kwa wakati.
"Sisi
kama wakulima wa Tunduru ukituambia tusitumie mfumo wa stakabadhi
ghalani hatukuelewi kwa sababu tunajua uzuri wa Mfumo wa stakabadhi
ghalani na ubaya wa ununuzi wa mazao kwa mfumo holela ",alisema.
Kwa
upande wake mkulima khadija Rajabu wa kijiji cha Ligunga Wilaya ya
Tunduru amesema licha ya wakati mwingine kujitokeza changamoto ya
kuchelewa kwa malipo bado mfumo wa stakabadhi ghalani ndiyo mkombozi wa
mkulima kwa sababu unalinda haki ya mapato ya mkulima.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...