Na Rahma Khamis- Maelezo Zanzibar 
Waislamu Nchini wametakiwa kushiriki katika kongamano la kilele cha sherehe za mwaka mpya wa kiislamu 1444 linalotarajiwa kufanyika tarehe 31 Julai mawaka huu ,katika Msikiti wa Jamiiu Zinjibar Mazizinim Zanzibar.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo huko Ofisini kwake Mazizini Zanzibar, Katibu wa Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema, waislamu waliowengi siku hizi hawafahamu mwaka mpya wa kiislamu jambo ambalo litapelekea kizazi kukosa kufahamu dini yao hivyo kufanyika kwa kongamano hilo litasaidia kufahamu mambo mengi yanayotokana na uislamu.

Ameeleza kuwa ni vizuri waislamu kujua lengo la uislamu na kuikumbusha jamii ili kuwa na tabia njema kwani unahimiza umoja, mshikamano , amani na heshima hivyo ipo haja kujitahidi ili kwenda sambamba na uislamu.

Aidha Mufti amefahamisha kuwa mwezi unaokuja wa Muharram ndio mwezi wa kwanza wa kiislamu hivyo Ofisi ya Mufti imeona ipo haja ya kufanya shamrashara kuelekea siku hiyo ambapo kutafanyika mambo mbali mbali ikiwemo uchangiaji wa damu salama katika Mnara wa kisonge.

Pia amefafanua kwamba kutakua na uzinduzi wa baraza la maulid katika Ukumbi wa Shekh IdrissaAbdulwakili sambamba na dhwafa itakayoanzia Msikiti wa Muembe Shauri na kumalizikia Bwawani.

Aliongeza kwa kesema kuwa tarehe 30 mwezi huu kutakua na ziara ya kutembelaea wagonjwa katika Hospitali ya mnazimmoja ili kudumisha umoja na mshikamano wa waislamu Nchini.

”Katika sherehe zetu tumeamua kufanya hivi ili waislamu wajue kwamba ni dini yenye kuhimizana watu kutendeana mambo mema katika jamii kwani tukifanya hivi wagonjwa watapata faraja kuona kuwa wanatembelewa na kujulikana halizao,”alisema KatibuMfaume.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo Hijra na Sensa ambayo itawasilishwa na Shekh Khamis Abdulhamid,Mtume kuhama Makka kuhamia Madina ambayo itawasilishwa na Shekh Othman Maalim,na Umuhimu wa elimu ambayo itawasilishwa na Sheikh Shaaban Batash Mjumbe wa Baraza la Ulamaa.
Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu 1444 ,huko Ofisni kwake Mazizini Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELZEZO ZANZIBAR.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...