Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ametoa siku 45 kwa taasisi za umma zinazodaiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Njombe (NJUWASA) kiasi cha fedha kinachofikia Milioni 280 kutokana na huduma ya maji iliyotolewa kwa taasisi hizo.


Kindamba ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye vyanzo vya maji vinavyohudumia wakazi wa mji wa Njombe chini mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Njombe na kuelezwa juu ya changamoto hiyo inayorudisha nyuma ufanisi wa mamlaka kutokana na madeni mbalimbali.


“Kwenye taasisi za umma tunadai karibu Milioni 280 kwa huduma ya maji tuliyoitoa na mara nyingi tunkavyodai madeni tunaambiwa bajeti imekuja pungufu ni kweli si rahisi bajeti ikaja kwa asilimia mia moja lakini tumejifunza wenzetu kwa huduma ya maji wanaweka kipaumbele cha mwisho”alisema Mhandisi John Mtyauli mkurugenzi wa NJUWASA


Kutokana na hili “Ninaelekeza listi ya taasisi hizi niletewe ofisini kwasababu huwezi ukawa unapewa huduma halafu hulipi na usipolipia maana yake unamkosesha huduma mtu mwingine,kama unajijua unadaiwa na mamlaka ya maji hakikisha unalipa deni lako ndani ya siku 45 na haijalishi wewe ni sekta ya Umma au binafsi nenda kalipe deni lako”amesema Waziri Kindamba




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...