Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango ameweka jiwe la msingi kituo cha afya Nsemulwa kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2021 kwa kutumia mapata ya ndani ya halmashauri ya shilingi milioni 400 na kikitarajia kuhudumia wakazi zaidi ya elfu kumi na nne wanaoishi eneo hilo.


Mradi wa Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya ulianzishwa na wananchi na  umelenga kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali teule ya rufaa mkoani katavi.


Akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa Mpanda mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho cha afya, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa Katavi kwa kudumisha amani pamoja na kufanya kazi kwa bidii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo iliopelekea kuzalisha chakula cha kutosha na ziada.


Amesema serikali itaendelea kusogeza huduma muhimu kwa wananchi kama vile maji, elimu na afya katika jitihada za kuboresha Maisha ya watanzania. Ameongeza kwamba  kwa sasa asilimia 90 ya dawa muhimu zinapatikana katika vituo  vyote vya afya nchini na kuwapongeza wote walioshiriki katika ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa kuiunga mkono serikali katika utoaji wa huduma za afya.


Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amekemea vitendo vya kuwakatisha wanafunzi wa kike masomo kwa kuolewa pamoja na kupata ujauzito. Amesema mkoa wa Katavi unaongoza kwa asilimia 40 kuwa na mimba za utotoni na kuwataka watendaji wote wa serikali, wazazi, viongozi wa dini na taasisi zote za kijamii kuungana kudhibiti vitendo hivyo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, mheshimiwa Dkt. Festo Dugange amesema katika manispaa ya Mpanda serikali imeendelea na ujenzi wa miradi yenye tija kwa wananchi kama vile ya afya, elimu na barabara. Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa magari mawili ya wagonjwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kutokana na changamoto iliopo ya upungufu wa magari hayo. Pia amesema pamoja na magari hayo serikali itapeleka mashine za X-ray nne katika mkoa huo ikijumuisha kituo cha afya cha Irembwe kilichopo Manispaa ya Mpanda itakayosaidia kupata huduma za kisasa za upimaji.


Awali Makamu wa Rais amezungumza na wananchi wa kata ya Katumba Kijiji cha Msaginya Jimbo Msimbo ambao walisimama barabarani kumsalimia. Amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kufanya kazi za uzalishaji ikiwemo chakula na kuwaahidi serikali haitaacha kupeleka fedha katika vijiji hivyo ili kuimarisha maendeleo ya wananchi katika sekta mbalimbali kama maji, elimu, afya na barabara.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa kata ya Katumba Kijiji cha Msaginya Jimbo Msimbo ambao walisimama barabarani kumsalimia akiwa ziarani mkoani Katavi Julai 21,2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Nsemulwa kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi tarehe 21 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Nsemulwa kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amara baada ya kuweka  jiwe la msingi tarehe 21 Julai 2022.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi na viongozi wa mkoa wa Katavi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Nsemulwa kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi tarehe 21 Julai 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na  viongozi  pamoja na wananchi wa mkoa wa Katavi mara baada ya kuhitimisha hafla ya uweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Nsemulwa kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi tarehe 21 Julai 2022.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa vikundi mbalimbali vilivyotumbuiza nyimbo za kuhamasisha sensa pamoja na ufanyaji kazi wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha afya Nsemulwa kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi tarehe 21 Julai 2022.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...