MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camilus Wambura amewataka wananchi wa jiji la Arusha kuendelea kutunza amani iliyopo na kutokujiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kipindi hiki ambapo kuna mkutano mkubwa wa Maras kutoka nchi saba za afrika mashariki.
IGP Wambura amesema hayo baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Arusha na kupokelewa na kamanda wa Polisi mkoani humo Justin Masejo ambapo aliwataka askari kuendelea kusimamia amani na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kutaka kuvuruga amani ya nchi.
Na kuahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...