Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 22 Julai 2022 ameshiriki ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa kuu katoliki la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili Jimbo la Mpanda mkoani Katavi. Ibada hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi Padri Leonard Kasimila.

Akizungumza na waumini mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaomba waumini na viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa na viongozi wake ili waweze kuwatumikia wananchi jinsi inavyompendeza Mungu na kufikia hatua ya juu zaidi ya maendeleo. Aidha amewasihi kuendelea kuliombea taifa amani kwa kuwa bila uwepo wa amani hakutakuwa na maendeleo yeyote.

Pia Makamu wa Rais amewaasa waumini wa kanisa hilo kujitolea kikamilifu katika kutunza mazingira ilikuepukana na athari mbaya zinazoweza kujitokeza kutokana na uharibifu wa mazingira. Amewaagiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ili kuwa na jamii bora itakayoweza kuliendeleza vema taifa.

Makamu wa Rais yupo mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi ambapo anakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamoto za wananchi katika mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akishiriki ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa kuu katoliki la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili Jimbo la Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 22 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa kuu katoliki la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili Jimbo la Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 22 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na baadhi ya waumini mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa kuu katoliki la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili Jimbo la Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 22 Julai 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...