Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAKUMBUSHO ya Taifa imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuzindua filamu ya Royal Tour ambayo kwao inakwenda kufungua fursa ya kuongeza watalii na wageni ambao watakuwa wakifanya utalii wa kutembelea maeneo ya makubusho ya taifa na malikale.

Akizungumza leo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt.Noel Lwoga amesema wanampongeza sana  Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuzindua filamu ya Royal Tour ambayo imeifungua nchi hasa katika eneo na utalii.

“Makumbusho ya Taifa katika maeneo ambayo tunayasimamia tuna faidika sana Royal Tour kwa mfano makumbusho zetu ziko katika miji mikuu ,hivyo  wageni wakifika wanashukua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam au wanashukia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro(KIA).

“Wanapofika kwenye miji hiyo mikubwa vivuto vikubwa wanavyonza kukutana navyo ni makumbusha yaliyopo kwenye ile miji, kwa hiyo tunatarajia kupata wageni wengi ambao watakuja kwenye makumbusho hizo.Hivyo tumejipanga kwasababu ukitembelea kwenye makumbusho zetu tunafanya maboresho ya kidigitali na kisasa zaidi.

“Tumejipanga kwasababu tunaboresha huduma katika makumbusho zetu ili kuweza kuwapokea hao wageni na kuwahudumia, vile vile katika maeneo ya Malikali ambayo yapo karibu na hifadhi za taifa watalii hawa wakifika maeneo ya hifadhni ni  dhahiri mvuto wa utalii unashabihishwa na maeneo ya malikale na maeneo ya utamaduni,”amesema.

Ameongeza kuwa mtalii anaweza kuingia hifadhi za taifa lakini akitoka anaingia na kwenye eneo la malikale , maeneo yote ya malikale.Hivyo wanaendelea kuyaboresha, kwa hiyo kimsingi wanaelekea kunufaika sana na Royal Tour na kwamba wanaendelea kujipanga vizuri kwa kuboresha miundombinu ili yaweze kupokea wageni na kuwahudumia.

Katika hatua nyingine Dkt.Lwoga amesema kwa ujumla Makumbusho ya Taifa katika kuendeleza utalii wameamua kuja na mkakati wa kufungua utalii wa miji kwa kuanza na Dar es Salaam kwa kuanzisha City Tour na katika maonesho haya ya sabasaba kesho Julai 9,2022 wanazindua utalii huo.

“Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi, tutapita katika maeneo takriban 18 ya Dar es Salaam ukiwemo Mji wa Kigamboni , Old Boma, jengo la Sultani ambao walinzisha mji huu wa Dar es Salaa, pia tutaona eneo ambalo Mzizima ilikuwepo , lakini makumbusho zetu mbili ikiwemo kijiji cha Makumbusho na tutakwenda mpaka Kunduchi.

“Pia kutakuwa na burudani katika kijiji chetu cha Makumbusho kwa maana ya kupata burudani ya ngoma asili.Tour hii tukumbuke itakuwa kila mwisho wa mwezi au katikati inategemea namna ambavyo utekelezaji wake utakavyokuwa kwa mwezi husika na itakwenda katika mji wa Arusha, Songea na Mmikindani ambako makumbusho za taifa zipo lakini kwa kuanza tumeamua kuanza na Dar es Salaam,”amesema Dkt.Lwoga.






Matukio mbalimbali katika picha baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt.Noel Lwoga kutembelea katika Banda la Makumbusho hayo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.Mkurugenzi huyo akiwa katika banda hilo amepata nafasi ya kuelezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na makumbusho hiyo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...