Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

BONDIA Karimu Mandonga anatarajia kupanda ulingoni tena Julai 30 mwaka huu dhidi Ya Mpinzani wake Shabani Kaoneka katika pambano la Raundi 6 kwenye Usiku Wa Deni (PAYBACK NIGHT) litakalofanyika Songea Mkoani Ruvuma.

Akizungumza Mandonga amesema amejipanga kuhakikisha anafuta makosa aliyoyafanya katika pambano lililopita na amemtaka mpinzani wake ajiandae kwani anaenda kukutana na kipigo Cha aina yake.

Kwa upande wake bondia Shabani Kaoneka amesema Mpinzani wake ni wakawaida hivyo ataendeleza alichokifanya Magambo Christopher Mkoani Morogoro kwa kumtwanga Ko.

Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni katika pambano la "PAYBACK NIGHT"litakalofanyika 30 Julai,2022 Songea mkoani Ruvuma huku pambano kuu siku hiyo kati ya bondia Selemani Kidunda "mtukazi" atakaye iwakilisha Tanzania dhidi ya bondia Erick Tshimanga Katompa kutoka Congo DR ambapo mabondia hao wanapanda ulingoni kwa mara ya pili kuoneshana ubabe baada ya pambano la kwanza kutoka Droo mwaka Jana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...