Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) wakiwa katika picha ya pamoja na cheti cha ushiriki wa maonesho ya vyuo vikuu yaliyohitimishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akipitia taarifa mbalimbali Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) katika maonesho yaliyohitimishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU), Maria Kisanko akizungumza katika maonesho yaliyohitimishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
CHUO Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) kimesema kuwa wameanzisha program ya shahada ya pili ya elimu katika mfumo wa kidigitali ambao unawawezesha walimu nchini kusoma katika vituo vyao vya kazi wakiwa wakipata taarifa zote za kusoma na kufundisha kwa kutumia Tehama.

Program hiyo imetokana na maoni ya wadau wa elimu wakiwemo wakuu wa shule ambao walishauri kuwe na mfumo wa kusoma huku wakiwa kazini.

Akizungumza wakati wa kilele cha maonesho ya Wiki ya Elimu ya Vyuo Vikuu yaliyoratibiwa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) Mratibu wa Masoko na Mawasiliano Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) Maria Kisanko amesema AKU itaendelea kutoa elimu bora nchini kutokana na mahitaji yaliyopo kwa kuzalisha wataalam wenye umahiri wa taaluma husika.

Aidha Kisanko amesema wanamategemeo ya kuanzisha shaada ya Uuguzi kwa wanafunzi wanaotoka moja kwa moja shuleni, kwani shahada ya Uuguzi iliyopo kwa sasa ni kwa ajili ya wauguzi walio na diploma ya uuguzi na wako kazini. Hii itaasaidia kuzalisha wauguzi kwa wingi kuliko ilivyo sasa.

"Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) tumejipanga katika kuendelea kutoa elimu bora kutokana na mahitaji ya wakati wa sasa Tanzania ili kuwa na wataalam kutokana na soko la ajira katika kada ya afya na elimu" amesema Kisanko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...