Afisa Mtendaji Mkuu wa African Guarantee Fund AGF, Jules Ngankam akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfuko wa uwezeshaji kwa wanawake wajasiriamali wadogo wadogo ukanda wa Afrika (AFAWA) jijini Dar Es Salaam.

Meneja wa AFAWA AfDB, Esther Dassanou akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfuko wa uwezeshaji kwa wanawake wajasiriamali wadogo wadogo ukanda wa Afrika (AFAWA) jijini Dar Es Salaam.
SERIKALI imeipongeza The African Development Bank’s Affirmative Finance Action for Women in Africa (AFAWA) Initiative kwa kuandaa mpango wezeshi wa kwanza wa fedha kwa ushirikiano na Mfuko wa Dhamana ya Afrika (AGF) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) utakao wasaidia wanawake kupata mikopo ya biashara na kuwawekea mazingira wezeshi ya uwekezaji
Mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano na Mfuko wa Dhamana ya Afrika (AGF) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA).
Akizungumza wakati wa uzinduziuzinduzi wa mfuko wa uwezeshaji kwa wanawake wajasiriamali wadogo wadogo ukanda wa Afrika (AFAWA) unaosimamiwa na African Guarantee Fund (AGF) kwa kushirikiana na AfDB leo Julai 26 2022, Naibu Waziri wa Uwekezaji , Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema kuwa Wizara yake inaunga mkono mpango huo utakao kwenda kuwasaidia wanawake ambao ndio kundi kubwa kwenye wajasiliamali nchini.
Amesema kuwa mpango unakwenda kuwakomboa kichumi kwa kuwa walikuwa wahanga wa kukosa dhamana kwenye mikopo mpaka kufikia hatua ya kuanzisha utaratibu wa kujikopesha wenyewe.
“ Hii ni fursa kubwa kwa kuwawezesha wanawake wajasiriamali wadogo na wakati, uzinduzi huu utapelekea kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini. Sisi kama serikali tutahakikisha tunasimamia fursa hii ili iweze kufika kwa walengwa, na kauli mbiu yetu ni wezeshi kwa wanawake kiuchumi". Amesema Kigahe.
Mkurugenzi Mkuu wa AfDB, Ofisi ya Maendeleo ya Kanda ya Afrika Mashariki na Utoaji Biashara Nnenna Nwabufo, amesema, kuna mikakati ya biashara ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wanawake, sio tu kwa taasisi za fedha na wajasiriamali wanawake, lakini pia kwa ukuaji wa uchumi mkuu.
Mtiririko huo wa Fedha unaendelea juu ya ushirikiano uliopo kati ya AFAWA na AGF ambao unalenga kuziba pengo kwa ufadhili la USD bilioni 42 kwa wanawake wajasiriamali wadogo barani Afrika. (WSME )
"Afrika Mashariki ni nyumbani kwa namna ya uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika. Mpango wa AFAWA unahakikisha wanawake wanaweza kupata fedha na mafunzo wanayohitaji ili kuchangia kikamilifu katika ukuaji huu". Amesema Nwabufo
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Mfuko wa Dhamana ya Afrika, Jules Ngankam amesema, “Afrika ni bara changa zaidi duniani, lakini wakati huo huo, nusu ya watu hao, idadi ya wanawake, bado iko mbali na kufikia uwezo wake katika kushiriki katika uundaji wa thamani. . "Tunapoanza safari hii ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wafanyabiashara wadogo na wa kati wanawake nchini Tanzania, kupitia mpango wa AFAWA wa Dhamana ya Ukuaji, tuna matumaini makubwa kuwa matokeo hayo yatakuwa makubwa,na ya muda mrefu na yatachochea ukuaji wa uchumi.” amesema
Naye, Esther Dassanou, Meneja wa AFAWA, amesema "AFAWA, kwa ushirikiano na Mfuko wa Dhamana ya Afrika, inafanya kazi moja kwa moja na taasisi za kifedha kote Afrika ili kuimarisha uwezo wao wa kuhudumia soko la wanawake, kuruhusu wanawake kuongeza biashara zao. Mfululizo wa Mtiririko wa Fedha wa AFAWA nchini Tanzania ni wa kwanza kati ya hafla kadhaa zinazofanana tunazopanga kuandaa kote barani Afrika ili kuonyesha taasisi za kifedha faida za kibiashara na kiuchumi za kufadhili wajasiriamali wanawake.
AFAWA na AGF zinakaribisha taasisi za fedha nchini Tanzania kujiandikisha kwa ajili ya mpango wa Dhamana ya Ukuaji. “Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina alipotembelea Tanzania Februari mwaka huu, alimuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa AFAWA itazinduliwa nchini,” Nnenna Nwabufo aliongeza. "Hii ni ahadi iliyotolewa na ahadi iliyotekelezwa. Nimefurahia sana kuwa sehemu ya hii."amesema
Naye Dkt. Zainabu Chaula Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amesema, wao kama wizara watahakikisha wanawake wanapata mikopo hiyo ili kuwawezesha kwenye shughui zao.
Amesema kuwa mpango huo unakomesha wanaweke kushindwa kuzifikia fursa za mikopo “kuna wanawake wengi wanatamani hizi fursa lakini hawazioni kwa hiyo kupitia mikopo ambayo AFAWA amewekeza pale ili kusiwe na mikingamano ya kokosekana mikopo”.
Amesema kuwa atasimama imara kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia wanawake wote nchini nzima kwa wao ndio walengwa wa mikopo hiyo “mimi nikiwa kama Katib Mkuu nitahakikisha hii mikopo inawafikia wahusika”.

Picha ya Pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...