Kamishna Msaidizi Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Irene Rugemalila akitoa elimu kwa Bi. Latifa Mohamed aliyetembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vjijini (IRDP) Bi. Martha Ambrose Qorro (kulia) akipewa kipeperushi na Afisa Ununuzi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Bi. Mwanaisha Mollel (kushoto) alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Siganike Baruti, Afisa Tehama - PPRA
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof. Martha Ambrose Qorro (kulia), akisikiliza maelezo kuhusu Taasisi ya Soko la Bidhaa (TMX) kutoka kwa Afisa Malipo na Uhawilishaji Bw. Prince Mng’ong’o alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mipango na Vijijini (IRDP) Prof. Martha Ambrose Qorro (kushoto) akipewa kipeperushi na Afisa Takwimu Msaidizi Bi. Neema Madembwe (katikati), alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Takwimu Msaidizi Bi. Mwanaabu Ngulumbi.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof. Martha Ambrose Qorro (kulia), akisikiliza kwa umakini maelezo kuhusu Mfuko wa SELF kutoka kwa Meneja Msimamizi wa Matawi wa SELF Bi. Cecilia Mwenisongole (kushoto), pindi alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo akikaribishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof. Martha Ambrose Qorro (Katikati), alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Prof. Hozen Mayaya.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Muktasi wa Wizara hiyo Bi. Mesia Msuya.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu Idara ya Sera kutoka kwa Mchumi Bi. Jesca Mugyabuso. kutoka Wizara ya Fedha na Mipango alipotembelea Banda la wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu Huduma ya Ununuzi Serikalini kutoka kwa Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Bw. Peter Mayile (Kushoto) kutoka Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) alipotembelea Banda la wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Takwimu wa GPSA Bw. Erasto Raphael.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu Huduma ya Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma kutoka kwa Mkuu Kitengo cha Manunuzi Bw. Stanley Jackson (Kushoto) kutoka Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA) alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na chou cha Uhasibu Arusha (IAA) kutoka kwa Afisa Uhusiano wa chuo hicho Bi. Sarah Goroi alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPBT) Bw. Amani Ngonyani (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa Bodi hiyo alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Chuo cha uhasibu Tanzania (TIA) kutoka kwa Mhitimu na Mjasiramali kutoka Chuo hicho Bw. Isaya Maligite alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Africa (AFCFTA) Mhe. Wamkene Mene akimkabidhi zawadi ya mshindi wa Tatu wa Jumla wa Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, Afisa Uhusiano wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Bi. Sarah Goroi yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifurahia baada ya kupokea zawadi ya mshindi wa Tatu wa Jumla wa Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, Iliokwenda kwa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Bi. Sarah Goroi, Kamishna Msaidizi Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Bi. Irene Rugemalila, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...