MBUNGE wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga amekutana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambapo ametoa semina kwa Wenyeviti na Makatibu wa Wilaya zote za mkoa huo kuhusu zoezi la Sensa, Kilimo na 10 Ujasiriamali.

Akizungumza katika semina hiyo, Mbunge Mayenga amewataka viongozi hao kuhamasisha zoezi la Sensa Kwa wananchi ili waweze kujitokeza na kuhesabiwa.

" Niwaombe viongozi wangu kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi wetu ili waweze kujitokeza na kuhesabiwa, zoezi hili ni muhimu kwetu maana linatoa fursa kwa Serikali yetu kujua idadi ya wananchi waliopo nchini ili iweze kupeleka maendeleo kulingana na idadi husika.

Rais wetu amefanya mambo makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tumeona anatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, anafungua Nchi, Mashirika makubwa ya Ndege yanatua nchini kuleta watalii jambo ambalo linaongeza Uchumi wetu.

Kwenye sekta ya elimu Rais wetu ameonesha yeye siyo tu kiongozi bali Mzazi, amefuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita leo hakuna Mtu analipa ada kwa watoto wetu kuanzia Shule ya msingi hadi kidato cha sita, hii ni kuonesha jinsi gani Rais wetu anataka kujenga Taifa la watu wasomi," Amesema Mbunge Mayenga.

Aidha Mbunge huyo amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa Chama ambapo amesisitiza viongozi wa CCM kumsemea Rais Samia kwa wananchi lakini pia kutoa elimu kwa wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la Sensa Agosti mwaka huu.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...