Raisa said,Korogwe

MBUNGE wa Korogwe Vijijini Mkoani Tanga Timotheo Mzava amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan Kwa kuwapatia shilingi bilion 3.8 Kwa akili ya Ujenzi wa daraja llinalounganisha kata mbili za Halmashauri ya Wilaya
ya Korogwe.

Ujenzi wa daraja hilo unatimiza ahadi yake ambayo aliyoitoa siku mbili kabla ya kuteuliwa kuwa Rais. Akielezea kuhusu daraja hilo wakati wa ziara yake katika eneo hilo linapojengwa daraja hilo,
amesema kuwa daraja hilo ni ukombozi.

Amesema kuwa mradi huo utachukua miezi 18 kukamilika na akamtakamkadarasi huyo aliyemtambulisha kwa jina la Nyanzi kuhakikisha mradihuo unakwisha kwa wakati na ikiwezekana hata kabla ya miezi hiyoiliyopangwa.

Mnzava alimsifia Rais Samia kwa kusikiliza kilio cha wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa wanapata tabu a kuvuka na kuhatarisha maisha yao kutokana na mto uo kuwa na mamba wengi wakilazimika kuvuka kwa kutumia boti.

Amesema akiwa pale alimwomba Mama Samia wakati huo akiwa Makamu wa Raisi ambaye aliagiza kiwekwe kivuko cha muda kuwasidia wananchi kuvuka katika eneo hilo.

Amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni pamoja ujenzi wa barabara kuweka changarawe kutoka eneo la Kwasunga hadi katika daraja hilo.

Mkazi wa Majengo, Mswaha, Zuberi Mbwana amesema wamepoteza watu wanofikia wanne kwa kuliwa na mamba. “Hata mimi nimeshadondoka na pikipiki hapa.kuna pikipiki kama mbili zipo ndani ya hapo hivyo ujenzi wa daraja hili ni nafuui kubwa kwetu,” alisema Mbwana.

Mkazi mwingine wa Mswaha Darajani, Miraji Athumani Msanga amesema kuwa wananchi walikuwa wanapata tatizo na hata wanawake walikuwa wanajifungulia hapo kutokana na changamoto ya daraja.

“Hapa ni kama makao makuu ya mamba. Watu walikuwa wanaliwa na mamba hapa. Ukivuka tu ni kama wanakutamani wanakuja. Watu walikuwa wanatozwa Sh 1,000 kuvushwa hapo katika kivuko lakini tangu ujenzi uanze naona hali inaanza kupungua,” alisema.

Naye Msimamizi wa mradi huo Joel Mkinga alisema walichelewa kuanza ujenzi kutokana mchakato wa kupata vibari .

“Tumemaliza kukusanya vifaa na ujenzi utakamilika Septemba, mwaka kesho,” amesema.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...