NA VICTORIA ROBERT KAHAMA

MKAZI wa kijiji cha Nyanholongo Wilayani Nyang’hwale mkoani Geita Nanuki Mathayo(25), amefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi wa Namba moja ulioko kijiji cha Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Katika ajali hiyo watu wengine wanne wamenusurika kifo baada ya kuokolewa na kukimbizwa katika kituo cha afya lunguya kwaajili ya matibabu kutokana majeraha waliyonayo.

Naye shuhuda wa tukio hilo, Doto Mabuli alidai kuwa ndani ya duara walikuwa zaidi ya watu watano wengine walikuwa wakichimba Dhahabu na yeye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuyasomba mawe hayo na kuyatoa nje bahati mbaya duara lilianguka akiwa anatoa mawe ndipo alipoanza kuowaokoa wenzake.

Mabuli alisema ndani ya Duara hilo kulikuwa na watu zaidi ya watu watano, lilipoanguka liliwafunika na baada ya hapo alifanikiwa kujinasua mwenyewe nakuanza kumwokoa aliyekuwa pembeni yake ambae likuwa amebanywa kichwa akinywa maji tu, baada ya kumnasua walisaidiana na wachimbaji wengine kuendelea kuwaokowa wengine.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Minele, Kijiji cha Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Kulwa Mathayo alisema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa mchana Julai 6,mwaka huu kwenye machimbo ya Namba 1. Kijiji cha Nyamishiga na kumtaja aliyefariki hapo hapo baada ya kupondwa na kifusi cha udongo ni Nanuki Mathayo (25) mkazi wa kijiji cha Nyanholongo wilaya ya Nyang’hwale Mkoa wa Geita.


Pia mwenyekiti huyo wa kitongoji hicho alisema kuwa katika ajari hiyo ni mmoja tu kafariki dunia kati ya watu watano waliokuwa wakichimba madini ya Dhahabu katika duara hilo na kuongeza kuwa wenzao wawili ni majeruhi wamelazwa katika kituo cha Lunguya kwaajili ya matibabu zaidi.

Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mgodi huo kwa sasa umesimama baada ya kuibuka kwa mgodi mwingine wa Nyamishiga ambao kwa sasa unamilikiwa na vikundi vya wanawake na hivyo katika mgodi huo vijana wa kijiji hicho wanachimba kwaajili ya kujipatia lidhiki.



Aliyesimama ni mwenyekiti wa kitongoji Kulwa Mathayo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya tukio cha mchimbaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...