Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mmoja miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele kuunga mkono harakati za uhuru wa Tanganyika Mzee Rehani Bilal Waikela aliyefariki dunia Jumapili 07 Julai 2022 jijini Dar Es Saalam.
Akizungumza katika ibada ya sala ya maiti iliyofanyika msikiti wa Kichangani Magomeni amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amemtaja Mzee Waikela kuwa mzalendo, jasiri mwenye uthubutu na mtu aliyejitolea kwa hali na mali katika kupigania Uhuru wa Tanganyika.
”Tumempoteza miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele katika kufanikisha uhuru wa Tangayika kwa sababu alikuwa jasiri, mzalendo mwenye uthubutu na utayari wa kujitolea nguvu na rasilimali zake wakati wa mapambano ya kutafuta uhuru, mchango wake ni mkubwa ambao chama na serikali tunauthamini na tutaukumbuka” Ndugu Samia Suluhu Hassan
Shaka aliwasilisha salam za pole za Chama Cha Mapinduzi kwa familia ndugu, jamaa, marafiki na kuwaomba kuwa wavumilivu na wenye subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Mzee Rehani Bilali Mwaikela amezikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam ambapo mbali na wanafamilia, ndugu na jamaa walihudhuria pia viongozi mbalimbali wa kisiasa pamoja na wanazuoni mashuhuri.
Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...