Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati akifungua mkutano huo tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akisistiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Omary Kipanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akionyesha Tuzo maalumu aliyotunukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa malezi bora kwenye Chama Cha SKAUTI Tanzania iliyotolewa wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mbeya Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati akifungua mkutano huo tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Na Janeth Raphael - Dodoma
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amewataka viongozi wapya wa Chama cha Skauti kuhakikisha wanatumia nafasi walionayo katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na vitendo viovu vinafanyika nchini.

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma Prof.Mkenda amesema kuwa kwa sasa matukio mengi ya utovu wa nidhamu na uvunjifu wa maadili mashuleni ni kutokana na kukosekana kwa michezo ambapo amewaagiza viongozi wa Skuti nchini kuhakikisha wanashughulikia suala hilo.

"Niwatake kushughulikia tabia hizi mbovu ambazo chanzo chake kikubwa ni kukosekana kwa michezo mashuleni enezeni Skauti mashuleni na kuhakikisha mnatoa malezi bora ili kuondoa haya matukio yanayosababishwa na malezi mabaya" Amesema Prof.Mkenda.

Mkenda amesema kuwa umefika wakati sasa kwa Uongozi wa Skauti kuonesha Uaminifu,uadilifu na nidhamu kwa kuhakikisha wanaondoa changamoto zilizopo na kufungua ukurasa wenye kusadifu kilichopo ndani ya chama hicho.

"Leo nafungua ukurasa mpya kwa kuwataka viongozi wa bodi ya skauti waliochaguliwa kuhakikisha wanalinda jina hilo lisichafuliwe na kuyaenzi yale yote yaliyoanzishwa na watangulizi ili kuendelea kuimarisha Uadilifu na nidhamu katika chama hicho" Amesema Prof Mkenda.

Kwa upande wake naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali zanzibar Ally Abdulgulam Hussein amesisitiza kufanyiwa Marekebisho ya Katiba ya chama cha Skaut nchini ili kuleta usawa,ufanisi wa kazi kwa misingi ya sheria, kanuni na Miongozo yake.

Skauti Mkuu Tanzania Bi.Mwantumu Mahiza ameishukuru serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa kuwapa eneo zuri ambalo litaenda kuleta Matokeo chanya katika chama cha skauti nchini huku Mdhamini wa chama cha Skauti Askofu Gervance Nyaisonga akawaomba viongozi watakaochaguliwa kuhakikisha chama kinasonga mbele pamoja nakuzingatia Nidhamu ya kazi.

Ikumbukwe kuwa Mkutano Mkuu wa Skauti Tanzania umeambatana na uchaguzi Mkuu ambapo wagombea wapo Tisa(9) na watakaopendekezwa na kupigiwa kura kati ya hao Tisa ni wagombea watatu(3) tu ambao Majina yao Yatapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na Amiri Jeshi Mkuu Samia suluhu Hassan ili amchague Skauti Mkuu Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...