Mjumbe wa MCT, Swaumu Mwalimu akizungumza katika uzinduzi huo.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAANDISHI wa habari nchini, wameaswa kupendelea kusoma vitabu na machapisho yanayochapishwa ili kukuza taaluma kwa vyombo vya habari na kuongeza uelewa.
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Juxon Mlay amesema hayo leo Julai 12, 2022 mkoani Dar es Salaam Salaam wakati wa uzinduzi wa machapisho manne ya vitabu yaliyoandaliwa na Baraza hilo la habari
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Jaji Mlay amesema, machapisho hayo iwapo yatasomwa yatawezesha waandishi kujenga uwezo na kuwasaidia katika kuandika habari zao kila siku na kwani machapisho mengi ni muhimu katika kuendeleza tasnia ya habari.
“Machapisho hayatakuwa na maana kama hayatasomwa, waandishi wa habari wanapaswa kusoma machapisho mbalimbali yanayochapishwa, habari yoyote iliyoandikwa haina maana kama haikusomwa,”amesema Jaji Mlay
Amesema Watanzania wanajenga utamaduni wa kutokupenda kusoma, lakini miongozo iliyotolewe ni muhimiu kwa waandishi kwani itawezesha kupata habari.
“Kama tukizingatia sheria hii na kufuata muongozo itatusaidia sana, machapisho mengine yametusaidia mfano ni namna ya kuandika habari kuhusu watoto, kwani iko sheria na mkataba wa kimatafa unaohusu haki za watoto,”amesema.
Vitabu vilivyozinduliwa ni Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari kwa mwaka 2020 hadi 2021 nchini Tanzania, Mwongozo wa Kupata na Kutoa Taarifa, Mwongozo wa Kuripoti Watoto na Kitabu cha kufundishia masuala ya jinsia na vyombo vya habari.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mkajanga amesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiandaa machapisho kwa kutumia wataalamu wa ndani na nje, kuhusiana na masuala ya vyombo vya habari.
“Kwa mwaka huu tumeanda machapisho manne ikiwemo muongozo wa kupata na kutoa taatifa kwa waandishi, wa hasabari na maafisa habari pamoja na muongozo wa vyombo vya habari wa kuandika habari za watoto,”amesema Mukajanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...