Balozi wa Kodi wa hiyari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Subira Mgalu ambaye pia ni Mbunge akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la TRA katika maonyesho ya 46 ya biashara ya Kimataifa sabasaba leo Julai 11, 2022 Dar es Salaam.
SERA za Mamlaka ya Mapato nchini TRA imetajwa kuwa chachu ya ongezeko la wawekezaji nchini baada ya kuzielewa sera hizo.
Hayo yameelezwa leo Julai 11 2022 na Balozi wa kodi nchini Subira Mgalu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la TRA wakati wa maonyesho ya 46 ya biashara sababa.
Mgalu amesema, Elimu inayotolewa na na TRA imefumbua macho wawekezaji juu ya elimu ya mlipa kodi ambayo imewavutia wawekezaji "Kwa taarifa nimepokea wananchi wamejitokeza lakini kipekee hata wawekezaji wemejitokeza kupata elimu ya mlipa kodi na baada ya maelezo hayo wawekezaji wamevutiwa kuwekeza nchini kwetu hili linakwenda sambamba na mpango wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan”
Aidha Mgalu amesema ameshuhudi kitengo cha maadili cha mamlaka hiyo ambacho kitawathibiti watumishi wa TRA ambao sio waaminifu .
“Kipo kitengo cha maadili ambacho kinatoa fursa kwa mlipa kodi kama wanaona mwenendo wa maofisa wanaoshughulika na kukusanya kodi sio nzuri wanakila sababu ya kutoa taarifa na zikashughulikiwa kama alivyosema Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba alipokuwa anawasilisha Bajeti ya Serikali alivyosema kuwa bado wapo wafanyakazi sio waaminifu wanaweza kutoa makadirio makubwa lakini wanaporuhusu mazungumzo yanashuka kwa hiyo natoa wito kwa walipa kodi kushirikiana na mamlaka hii”
Amebainisha kuwa kwenye idara ya sera na utafiti ya mamlaka hiyo itakuwa ikitafiti namna ya kuongeza walipa kodi na kupunguza walipa kodi wachache wanaolipa kodi nyingi.
Kuhusu elimu kwa mlipa kodi Mgalu ametoa wito kwa watanzania kudai risiti kwa kila manunuzi huku wafanyabiashara wakitoa risiti kwa kila wanapofanya mauzo.
“Kwa namna ambavyo watanzania wanaelimika katika kulipa kodi , tumeanza mwaka mpya wa fedha ambao serikali inatarijia kukusana shilingi Tirioni 41.48 ili ituletee maendeleo kwenye sekta mbalimbali “
Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo imepewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi Tirioni 23 na kwamba pesa hizo ndio zitakazojenga miradi mbalimbali ya kimkakati na elimu bure, pamoja na utoaji wa huduma za afya na miundombinu mbalimbai nchini.
Kuhusu vitambulisho vya Taifa NIDA Mgalu ametoa wito kwa watanzania kuhakikisha wanapata vitambulisho hivyo ili kuongeza wigo wa walipa kodi kwa itakuwa na TIN namba itakayotoa tathimin walipa kodi.
Kwa upande wake, Peter Kipapa Ofisa muelimishaji wa TRA amesema kuwa kitengo hiko kimetembelewa na wageni wengi waliokuwa wanataka kujua namna ya ulipaji kodi nchini tanzania na kwamba wanaonesha kuridhishwa na utendaji wa mamlaka hiyo.
“tumepata wageni wengi waliotaka kujua elimu ya kodi hapa Tanzania kwa namna gani wanaweza kulipa kodi na faida au misamaha ya kodi watakayoipata watakapokuja kuwekeza na wameridhishwa na maelezo yetu” amesema Kipipa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...