Na Chalila Kibuda , Michuzi TV
"Kazi ni kazi na hakuna kazi aliyopangiwa kufanya mwanaume hivyo kila mtu anaweza kufanya kazi kwa kazi yeyote inayoweza kuzalisha kipato haina ujinsia"
Hayo ni maneno ya Jackline Meshack ni mwanafunzi , Mhitimu na Mwalimu Msaidizi wa masuala ya Urembo na Kinyozi Chuo VETA Shinyanga.
Jackline akizungumza katika Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam amesema wasichana kazi ya kuwa vinyozi wamewaachia wanaume hali iliyomfanya ajufunze aende darasani kujifunza urembo na kunyoa ambapo alifanikiwa.
Amesema sasa anaweza kunyoa kila aina ya unyoaji kadri ya mtu anavohitaji na akitoka kuweza kufurahia kazi iliyofanyika.
Amesema wasichana wasiache kazi na kusema za wanaume kwani baadhi ya wanaume hao wanapenda wanyolewe nywele na wanawake hali ambayo ni fursa ya kutengeneza kipato kama msichana au mwanamke.
Amesema kuwa watu siku hizi wananyoa nywele na kuhitaji kutengeneza uso ambapo ni kazi mbili ambayo kila moja ina malipo yake lakini baadhi wasichana wanajikita katika kutengeneza uso tu bila kujifunza kunyoa.
Jackline amesema VETA inatoa mafunzo hayo katika baadhi ya vyuo hivyo wasichana waende wakajifunze huko.
Mhitimu wa VETA Shinyanga Jackline Meshack akionesha umahiri wa Unyoaji Nywele kwa mteja katika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...