TIMU ya Gofu ya klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo imewasili Mkoani Arusha kushiriki michuano ya (Kilimanjaro Open 2022) iliyoanza kutimua vumbi mapema leo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Isiaka Daudi ambaye hivi karibuni amekua bingwa wa TFS Lugalo Open ameendelea kutamba baada ya kupiga Mikwaju 77 huku akiahidi kufanya vizuri zaidi na kurudi na Ushindi Lugalo kwa siku ya kesho.

Upande wa wanawake Mchezaji Zainabu Bachoo kutoka Lugalo amesema Mashindano ni Magumu kwa kuwa no mara yake ya Kwanza lakini amefurahia kucheza na Wachezaji Wakongwe

Kwa Upande wa wachezaji wa kulipwa waliofungua Shindano Ijumaa, Jimmy Mollel wa Arusha ameongoza akifuatiwa na Frank Mwinuka wa Lugalo baada ya kufungana kwa mikwaju 155 na kulazimika kurudia Uwanja Mmoja na Kufungwa kwa Mkwaju Mmoja.

Shindano hilo linalofanyika klabu ya Kilimanjaro Gofu klabu Jijini Arusha litahitimishwa kesho Jumapili julai 10, 2022 sambamba na zoezi la ugawaji zawadi kwa watakaofanya vizuri zaidi ya wenzao.

Wachezaji kutoka vilabu mbalimbali ikiwemo Klabu ya jeshi lugalo gofu ikiendelea na Michuano ya Kili open 2022 inavofanyika Mkoani Kilimanjaro ambapo inatarajiwa kufungwa  julai 10 na washindi watakaofanya vizuri kupatiwa zawadi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...