WAJUMBE wa Halmashauri ya kijiji cha Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wamemtuhumu Diwani wa kata hiyo Benedicto Manwari kujinufaisha na raslimali zinazotokana na mgodi huo na kijiji kutoona manufaa yoyote.
Wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo wamesema pamoja na Mgodi huo bado kijiji kinakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo ubovu wa miundombinu ya bara bara, ukosefu wa nyumba za walimu pamoja na huduma zingine.
“Kulingana na kijiji chetu kubarikiwa kuibuka kwa migodi tulijipanga kama serikali ya kijiji tusimamie wenyewe baadhi ya shughuli mgodini ili tufanye maendeleo ya kijiji chetuikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu lakini Diwani akaingilia akidai atatusimamia yeye kama diwani lakini hatuoni faida ya mgodi pamoja na kukusanya kiasi cha fedha ambazo diwani anazing’ang’ania, amesema Lenatus Clementi.
Aidha alituhumu kuwa katika mfuko huo wa kijiji wakikusanya shilingi milioni tatu kama kwenye maduara waliyokabidhiwa kijiji kama yalivyo makubaliano ya mgodi na kijiji Diwani huyo anakiachia kijiji kiasi cha shilingi laki moja ama mbili zingine anapeleka Katani jambo ambalo linawafedhehesha.
“Shule haina nyumba za walimu, wanatembea umbali mrefu kutoka Kata ya Lunguya na Kata jirani ya segese kuja kufundisha watoto wetu, kijiji hakina maendeleo miundombinu ya barabara majengo ya shule nayo hayatoshi leo fedha hizo zingeweza kusaidia kupunguza kero lakini Diwani anabeba hela zote na hata kuko hatujui fedha anazipeleka wapi wakati hata kata yenyewe haina maendeleo,” Wamelalamika wajumbe wa serikali ya kijiji cha Nyamishiga.
Wamesema kuwa Kata ya Lunguya imekuwa na migodi mingi ambapo Diwani huyo amekuwa akijinufaisha yeye binafsi
Akijibu malalamiko hayo Diwani wa Kata ya Lunguya Benedicto Manwali amesema kwa sasa mradi uliopewa kipaumbele katika kijiji hicho ni sekta ya afya ambapo kunaukamilishaji wa Zahanati ya kijiji na miradi mingine itafuata baada ya hapo.
“Tunajenga nyumba ya mganga Two in One pamoja na kumalizia ujenzi wa Zahanati ya kijiji ili wananchi watibiwe pale lakini tutakarabati majengo ya shule ya msingi Nyamishiga na kujenga nyumba za walimu, kweli zilizopo ni hazifai ni zamatope ndiyo maana walimu wanaonekana kuzikimbia,”amesema Benedicto Manwari.
Baadhi ya wajumbe wa halmashauri ya kijiji wakiwa wameketi nje ya jengo la ofisi ya kijiji cha Nyamishiga baada ya mahojiano na waandishi wa Habari.
Pichani ni Diwani wa kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama, Benedictor Manwari akijibu tuhuma zinazomkabiri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...