Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani  ACP Gregory Mushi akionyesha nyaya za umeme za TANESCO ambazo zimeharibiwa na watu wasiojulikana Wilayani Kibaha  Mkoani Pwani.
Mwenye suti nyeusi ni Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Pwani Mohammed Mtoro

Na Khadija Kalili, Pwani
SHIRIKA la Umeme Tanzania, Mkoa wa Pwani limepata hasara ya zaidi ya Shilingi Mil.76 zilizo sababishwa na mtu mwenye nia ovu kuharibu kwa makusudi miundombinu ya TANESCO.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Afisa Kitengo Cha Usalama (TANESCO) Mkoa wa Pwani Mohammed Mtoro amewataka wananchi mkoani hapa kuwa walinzi wakuu wa miundombinu na kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Afisa huyo aliyasema hayo kufuatia uharibufu wa miundombinu uliofanyika kwenye stendi kuu ya magari ya Mkoa iliyopo Wilayani Kibaha baada ya watu wasiofahamika kuiba nyaya za taa kwenye stendi hiyo.

Kaimu Kamanda Mkoa wa Pwani ACP Gregory Mushi amethibitisha hayo alipozungumza leo asubuhi Julai 5 alipozungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani Kibaha kuwa wamemkamata mtu mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Mlandizi kati akiharibu miundombinu ya TANESCO kwa kukata line ya umeme ya msongo wa 33KV ambao ulikuwa unamhudumia mteja aliyefahamika kwa jina moja la Swai.

"Mbinu iliyotumika ni kwamba nguzo ilichomwa moto na kusababisha line hiyo kuanguka na kuiba waya wa aluminium ACCR 100 MM2 na kusababisha Shirika hasara ya Tsh.76,896108.22(Milioni Sabini na sita laki nane tisini na sita elfu miamoja na nane na Senti ishirini na mbili)" alisema Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani Mushi.

Aidha Kaimu Kamanda aliongeza kwa kusema kuwa Julai 3 mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni Mdaula Wilaya ya Kipolisi Chalinze Jeshi la Polisi likiwa katika msako na operesheni mbalimbali lilimkamata mtu mmoja mwanaume miaka 48 mkazi wa Makambako Iringa akisafirisha mirungi bunda 150 zenye uzito wa kg 70 kutoka Wilayani Mkoani Kilimanjaro kuelekea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe kwa kutumia kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.254 DDY aina ya Toyota Ipsum.

Kaimu Kamanda huyo alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto Rachel Michael mwenye umri wa miaka Saba aliyebakwa na kuuawa Mei 30 mwaka huu katika eneo la Misugusugu Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Wakati huohuo Kaimu Kamanda aliongeza kwa kusema kuwa katika kipindi cha wiki mbili kuanzia Juni 21 Hadi Julai 4 mwaka huu walifanya misako na operesheni na kufanikiwa kumkamata na kuokoa vitu mbalimbali ambavyo ni betri 8 za sola, vipande8 vya nguzo za taa zilizokatwa,box la kutunzia sola,praiz na kisu, mtungi wa gas, pikipiki moja aina ya TVS isiyo na namba ya usajili.

"Vitu vingine vilivyokamatwa ni Nyaya za kupitishia umeme za almonium,televisheni mbili,bhangi gunia mbili, vifurushi viwili,Puli 9 na kete 187,madawa ya kukevya aina ya Heroine kete 110 na pombe ya Moshi (Gongo) Lita 43.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa Rai kwa wananchi wote kuishi kwa kufuata misingi ya sheria kwani kuihujumu miundombinu ya Taifa kwani ni hasara Kwetu sote na siyo mtu mmoja pia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya kwani ni hatari kwa afya zao na jamii kwa ujumla" alisema ACP Mushi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...