NA FARIDA SAID, MOROGORO.

BARAZA la tiba asili na tiba mbadala nchini limepiga marufuku  matumizi na kuifutia usajili dawa ya  Hensha maarufu kama MKONGO iliyokuwa na namba za usajili TZ17TM0027  inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic kilichopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Morogoro Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Hamis Masanja Malebo ameleza sababu za kufungiwa kwa dawa hiyo ni kutokana na dawa hiyo kuchanganywa na dawa nyingine ya kisasa aina ya Viagra  

Alisema baraza lilibaini dawa hiyo ya Hensha alimaarufu Mkongo ilikutwa imechanganywa na dawa ya iitwayo Slidenafil kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.

 

Aidha kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha inaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo ya Mkongo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki Emmanuael Maduhu.

 

 Alisema baraza lina wajibu wa kuziondoa dawa ambazo usalama na ubora wake haupo katika viwango sahihi kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 13(1) cha kanuni ya dawa asili ya mwaka 2008.

 

Mwenyekiti huyo wa Tiba asili na Mbadala alisema kwa mganga ambaye anahitaji kutangaza dawa yake ni lazima afuate utaratibu wa kusajili dawa kwa kupima ubora, usalama na baade kuomba kibali cha  matangazo kutoka baraza.

 

 Aidha  amewataka wananchi pamoja na kutumia tiba lishe zinazoboresha afya kuzingatia taratibu na kanuni za afya ili kujikinga na maradhi ya aina mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...