Dkt. Sharif Luwena, wa Taasisi ya Mifupa Moi, akimuonyesha mmoja wa mwanchi aliyetembelea banda la Taasisi ya Mifupa, Moi wakati Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, mfano wa uti wa mgongo.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
BAADA ya kukithiri kwa malalamiko ya watu wanaosumbuliwa na matatizo ya magoti Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) imeanzisha operesheni ya viungo hivyo bila kumfanyia mgonjwa upasuaji
Daktari wa Taasisi hiyo, Sharif Luwena, ameyasema hayo leo Julai 9, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo inayoshiriki maonyesho ya 46 ya biashara ya sabasaba ya mwaka 2022 wamewasikia watu wengi wakilalamika juu ya maumivu ya Magoti.
“Miongoni watu tuliowaona hapa ni wagonjwa wa magoti , watu wanaokuja hapa wanalalamika maumivu ya magoti na wanasema wamekiwa wakiekwenda Hospitali mbali mbali na ku aambiwa hawana tatatizo lolote …tunawashauri kufika MOI kufanyiwa uchunguzi yakinifu”.
"Wagonjwa wengi wakienda kwenye hospitali zingine za pembeni huwa wanafanyiwa Xray, kipimo ambacho ni cha awali kabisa kwenye shida ya goti ambacho kinaonyesha mifupa tu ya goti lakini kipimo ambacho mgonjwa anakuja kupimwa Moi ni kipimo cha MRI ambacho pamoja na mifupa kinaonyesha pia nyama nyama ambazo zipo kwenye goti na sehemu zote ambazo mara nyingi ndizo zinakuwa na shida kuliko mifupa". Amesema Dkt. Luwena
Amesema kuwa mgonjwa atapimwa kwa kipimo cha (MRA) “Operesheni itafanyika bila kupasua goti tunatoboa matundu tu baada ya muda mgonjwa atakuwa mzima kabisa”.
Luwena amesema kuwa tatizo la Magoti si la kupuuzwa kwani kadri umri unavyoongezeka ndivyo tatizo linavyoongozeka na kwani ukiacha wale wanaopata matatizo ya Magoti kwa kutumia kwenye ajali ama mazoezi, wagonjwa wengi hupata tatizo hili kwa sababu ya ongezeko la umri na kwamba watu wenye Umri kuanzia miaka 55 wamekuwa wahanga wa tatizo hilo.
Ameeleza athari za tatizo la magoti lisiposhughulikiwa kwa wakati linaweza kumsababishia mgonjwa kushindwa kutembea ambapo kunapelekea mgonjwa kuwekewa magoti bandia amabayo yanagarimu mpaka shilingi Milioni kumi.
“Athari ipo tena ni kubwa kadri siku zinavyokwenda tatizo linakuwa kubwa mifupa ikisigana magoti yanalika ambapo ukija kwetu tunafanya operesheni kubwa ambayo inagharimu shingili 5 hadi 10 milioni” amesema Luwena.
Luwena ametoa rai kwa wananchi kujitokeza mapema kabla athari za ugonjwa huo hazijawa kubwa.
Dkt. Sharif Luwena, wa Taasisi ya Mifupa Moi, akimuonyesha mmoja wa mwanchi aliyetembelea banda la Taasisi ya Mifupa, Moi wakati Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, chuma cha nje anachowekewa mgonjwa alievunjika mfupa wa mguu (Tibia) Kitaalam kinaitwa Ilizarov Extenal Fixato.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...