Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA kuwa utabili unaonesha kuwa mwaka huu kwa wale wasiopata watoto kwa muda mrefu watafanikiwa kupata watoto salama na watoto wengi watazaliwa lakini pia watoto hao watapata huduma stahiki Serikalini, majumbani, kwenye jamii na hata kutoka kwenye Ofisi binafsi.

Utabili huo ulitolewa Jijini Dar es Salaam na Dkt. ambaye pia ni Tabibu wa Tiba Asili kwa kutumia Miti Shamba kutoka Mkuranga Kilimahewa Kassinu Mswahili.

Alisema "utabili wa mwaka huu 2022 unaonesha una neema kwa wanawake wote ambao hawajapata watoto kwa muda mrefu mwaka huu watapata ujauzito na watajifungua watoto,"alisema Dkt. Mswahili.

Mbali na hilo pia alisema kuwa mwaka wa wauguzi, waganga au Madaktari watagundua ugonjwa mpya kabisa wa binadamu, mifugo au wanyama kwa ujumla.

"Mbali na hilo pia itagunduliwa dawa mpya ya magonjwa ambayo kwa muda mrefu yamesumbua jamii kwa namna moja ama nyingine," alisema na kuongeza;

"Nawashauri Watabibu, waganga, wauguzi na madaktari wote wajitahidi kufanya kazi kwa weledi ili kufanikisha na kuisaidia jamii,".

Alisema pia mwaka huu watanzania watapata mafanikio makubwa hasa kwenye uongozi huu wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Aidha, alisema anapenda kumpongeza sana Rais kwa jitihada zake anazozifanya kwa ujenzi wa Taifa na kuwaletea wananchi maendeleo makubwa..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...