Na Victoria Robert Kahama -Shinyanga
Mkazi mmoja wa kata ya Mhungula wilayani kahama mkoani Shinyanga ameshikiliwa na na Jeshi la Polisi Wilayani humo kwa tuhuma ya kumpa ujauzito mwanafunzi wadarasa la saba(14) katika shule ya msingi Mhungula ambae jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa serikali za mtaa wa Inyanga katika kata ya Mhungula Nestory Bungola wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amemtaja kija huyo aliyejulikana mmoja la Joseph ambae anadaiwa kuwa ni mkaanga chips katika eneo lake ambae ndie aliyedaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo ambae anaishi nae katika nyumba mmoja jambo lililopelekea kukatisha masomo yake.
Aidha mwenyekiti huyo alidai kuwa wazazi wa kijana wamekuwa wakimfuata mzazi wa binti kwa kutaka wayamalize jambo ambalo mwenyekiti alimkemea mzazi wa binti kujihusisha na masuala ya rushwa jambo ambalo nikinyume cha sheria badala yake waache hatua kali zichukuliwe dhidi ya kijana huyo ili iwefundisho kwa wengine wenye tabia hizo.
Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Fatuma Hamisi amesema kuwa amegundua hali ya ujauzito wa mwanae ukiwa tayari umefikisha miezi nane ambapo mwanafunzi huyo hajahudhuria masomo tangu mwezi wa tatu mwaka huu.
Mama
mzazi wa mwanafunzi(kulia) akizungumza na waandishi wa habari



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...