Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la NIC katika Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*Ashauri waendelee kutoa elimu pamoja na Sekta ya Utalii
Na Chalila Kubuda , Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amelipongeza Shirika la Taifa la Bima (NIC) kwa kazi nzuri wanaotoa katika sekta ya bima.
Masanja aliyasema hayo wakati alipotembelea Banda la NIC katika Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema katika soko la bima kuna ushindani mkubwa hata sekta ya Maliasili na Utalii ni wadau bima.
Aidha amesema katika ushindani na kuongeza kuwa waendelee kutoa elimu ya bima katika sekta zote kwani bima ina umhimu katika ulinzo biashara na mali.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu ya bima ikiwa ni katika ushiriki wa maonesho mbalimbali ambayo yanakusanya wananchi kwa wakati mmoja.
Aidha amesema sekta ya utalii watakwenda kwa kugusa kila mdau wa sekta hiyo kuwa na bima kutoka NIC kwani wanachakata madai ya mteja ndani ya muda mfupi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...