Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Anthony Mavunde ameitaka Taasisi ya Utafiti Kilimo(TARI) na wadau wengine wa kilimo kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kumsaidia mkulima wa Tanzania kulima kwa tija.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Hombolo-Jijini Dooma wakati akitembelea mashamba ya mtama yanayofanyiwa majaribio kwa mbolea kutoka kiwanda cha ITRACOM FERTILIZERS kinachojengwa Nala,Dodoma.

“Mh Waziri Bashe alitoa maelekezo kwamba wataalamu wa TARI na TFRA mkae pamoja na kiwanda ili kufanya majaribio ya mbolea hii kutokana na ikolojia ya nchi yetu ili mbolea itakayozalishwa iweze kukidhi mahitaji ya udongo wa mbalimbali ya nchi.

Leo nimekuja hapa kushiriki zoezi hili la kutembelea mashamba ya mtama ya majaribio kujionea jinsi mbolea hii inavyofanya kazi katika zao la mtama.

Wadau wa kilimo mna wajibu wa kuielimisha jamii juu yaa matumizi sahihi ya mbolea kwa lengo la kuinua kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao yetu.

Katika kuchochea matumizi ya mbolea,serikali itatenga Tsh 150bn kama ruzuku ili kumpunguzia mzigo wa bei mkulima,sambamba na kuchochea ujenzi na uanzishwaji wa viwanda vya mbolea nchini”_Alisema Mavunde

Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt. Geoffrey Mkamilo amesema zoezi la kufanya majaribio ya matumizi ya mbolea zitakazozalishwa na Kiwanda cha ITRACOM limefanyika katika vituo vinne vya TARI katika ikolojia tofauti na kwamba mbolea hizo zimeonekana kuwa na ubora mkubwa katika kukuza mazao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha ITRACOM Fertilizers Ndg. Nduwimana Nazaire amesema kwamba kiwanda hicho cha mbolea kitaanza uzalishaji rasmi mwezi wa 7/2022 na kwamba matumizi makubwa ya malighafi yatakauwa ni ya samadi na hivyo kutoa rai kwa wafugaji nchini Tanzania kuchangamkia soko la kusambaza samadi kiwandani hapo.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...