Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Yanga rasmi wameridhia azimio moja la kumpitisha Mgombea pekee wa nafasi ya Urais katika Klabu hiyo, Eng. Hersi Ally Said kuwa Rais wa Klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu, Malangwe Ally Mchungahela amesema kutokana na Mgombea huyo kuwa peke yake katika nafasi hiyo, Kanuni ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) Kanuni 23 (9) imeelekeza kuwa endapo kutakuwa na Mgombea pekee Wanachama watapisha azimio kwa kupiga Kura za Ndio au Hapana.
Eng. Hersi anakuwa Rais wa Klabu hiyo akichukua Kiti kilichoachwa wazi na Dkt. Mshindo Msolla ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo kabla ya kujiuzulu kwenye Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) jijini Dar es Salaam.
Jumla ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu 805 kutoka Matawi 161 ya Klabu ya Yanga, watapiga Kura kuwachagua Makamu Rais wa Klabu, mmoja kati ya Mwanamama Suma Mwaitenda na Arafat Haji, Pia watapiga Kura kuchagua Wajumbe wengine watano wa Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...