Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amelidhishwa na hali ya upatikanaji wa huduma ya maji alipoongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, wakuu wa wilaya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani walipotembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na hali ya uzalishaji wa maji katika Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Makalla amesema wamekuja kukagua vyanzo vya maji pamoja na hali ya upatikanaji wa maji ukoje na kuendelea kukagua upatikanaji wa maji ili kujionea uhalisia wa vyanzo vya maji hasa kwenye Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini.
"Mimi na wenzangu tuliofanya ziara leo tumejiridhisha pasipo mashaka kuanzia Ruvu Juu mpaka huku Ruvu Chini tumeona kwamba hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa unaridhisha maana yake ni kwamba zipo jitihada zimefanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA)"Alisema Makalla
Pia Makalla amesema DAWASA chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja wameweza kujenga bwawa la kuhifadhia maji hivyo jitihada hizo zinapaswa kufungwa mkono na wadau mbalimbali nani jukumu viongozi wa Mkoa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuwajibika katika kulinda vyanzo vya maji ya mto Ruvu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema wametembelea Ruvu Juu na kuona kina cha maji ni mita 16.5 na Ruvu Chini ni mita 4.2 ambapo kitaalam ni maji yanayotosheleza.
"Kuna viashiria vimetuonesha inabidi tuchukue tahadhari maana tumepata taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu upungufu wa mvua kwa mwaka huu hivyo inabidi kusimamia vyanzo vya maji ili kuweza kuvuka salama kwenye kipindi cha ukame" alisema Kunenge
Amesema anafahamu watu wa Bonde wanatoka huduma vizuri ila inabidi kusimamia vizuri utowaji wa vibali kulingana na mahitaji kwa kuzingatia vipaumbele kwa ajili ya matumizi ya binadamu na Kwa wakati huu mmeanza kusitisha shughuli mbalimbali za uzalishaji kwenye mashamba ya Wananchi ili kuweza kupatikana maji yatakayohudumia Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Pia Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema wameweza kutengeneza bwawa la kuhifadhia maji ambalo kitawezesha kufika salama kwenye mwezi wa Tisa na wa kumi.
Pia anasema Nia ya ziara ni kuweza kuangalia vynazo vya maji pamoja na mifumo ya uzalishaji wa maji kwenye Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini inayohudumia Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla , Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari
Kunenge, wakuu wa Wilaya Pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama kuhusu
kazi zinazofanywa kwenye Mtambo wa kusukumia wa maji wa Ruvu Juu wakati
wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na
Pwani kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na
hali ya uzalishaji wa maji wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ya kutembelea na kukagua
Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu leo
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla , Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari
Kunenge, wakuu wa Wilaya Pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama kuhusu
namna uzalishaji wa maji wa Ruvu Juu unavyofanyika chini ya usimamizi wa
DAWASA wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es
Salaam na Pwani kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanyika pamoja na hali ya uzalishaji wa maji wakati wa ziara ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ya
kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu
Juu leo.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ikiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Abubakari Kunenge wakiendelea kukagua na kujionea uzalishaji maji katika
Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya
kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu
Juu leo Mkoani Pwani.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani(RAS)
Injinia Hajat Mwanasha Tumbo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian
Luhemeja pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakinywa maji yanayozalishwa DAWASA
katika Mtambo wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea
shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na hali ya uzalishaji wa maji
wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam
na Pwani ya kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu
Chini na Ruvu Juu leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akisaini kitabu mara baada ya
kuwasili kwenye Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya
kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na hali
ya uzalishaji wa maji wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ya kutembelea na kukagua Mitambo ya
Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akisaini kitabu mara baada ya
kuwasili kwenye Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya
kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na hali
ya uzalishaji wa maji wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ya kutembelea na kukagua Mitambo ya
Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu leo.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ikiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Abubakari Kunenge wakiendelea kukagua na kujionea uzalishaji maji katika
Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini wakati wa ziara ya Kamati hiyo
ya kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu
Juu leo Mkoani Pwani.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanyika pamoja na hali ya uzalishaji wa maji wakati wa
ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
ya kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu
Juu leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza na wandishi wa habari
mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanyika pamoja na hali ya uzalishaji wa maji wakati wa
ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
ya kutembelea na kukagua Mitambo ya Kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu
Juu leo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu namna DAWASA ilivyojipanga kutoa huduma Kwa wananchi bila
changamoto yoyote wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wa Dar es Salaam na Pwani walipotembelea Mitambo ya uzalishaji maji ya
Ruvu Juu na Ruvu Chini kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika hapo
pamoja na hali ya uzalishaji maji katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa
wa Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...