Asila Twaha, Dar es Salaam

Tamisemi Queens inaendelea kufanya vizuri kwa kuwasha moto uwanjani katika mchezo wa netibloli ligi daraja la kwanza na kuzichapa magoli timu zilizoshiriki michezo hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akihojiwa Julai 14, 2022 kocha wa timu hiyo Bi. Maimuna Kitete amefichua siri ya ushindi huo kuwa ni kufanya mazoezi kwa bidii na maarifa ambapo inawasaidia wazidi kuwa wazuri katika michezo, lakini pia uwepo wa utayari kwa wachezaji hao katika kujituma na kukubali kwa kile wanachoelekezwa kutoka kwa viongozi wao kwa kuwa na nidhamu ndani ya michezo na nje ya michezo.

Maimuna ameushukuru uongozi kwa ushirikiano wanaoupata kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI katika kujali na kuthamini juhudi zao katika michezo inawafanya waendelee kufanya vizuri zaidi.

Timu ya Tamisemi Queens imeifunga goli 51-21 Nyika leo ambapo mchezo huo ulichezwa mara mbili jana ulichezwa kwa nusu saa lakini kutokana na umeme kukatika uamuzi uliotolewa na wasimamizi wa mchezo huo kuendelea kumalizika leo asubuhi na timu ya Tamisemi Queens kufanikiwa kuwafunga goli 51 wapinzani wao timu ya Nyika.

Naye Kapteni wa Timu Dafroza Luhwago amewaomba viongozi na mashabiki kuendelea kuwaombea na kuwasaidia bila kuchoka na kuwahakikishia timu hiyo kuendelea kufanya vizuri kwani mpaka sasa wameshacheza timu nne na timu zote hizo wameshinda vizuri kwa kuwa katika nafasi nzuri.

Aidha, leo tarehe 15 Julai, 2022 timu ya Tamisemi Queens imepangwa kucheza na timu ya Polisi Morogoro katika uwanja wa ndani uliopo ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...