Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Pwani Julai 26, 2022.
Baadhi ya wakufunzi wa Sensa wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika Mafunzo.Na Khadija Kalili Kibaha
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka Makarani wa Sensa wa kuzingatia kanuni sheria na taratibu ili zoezi hilo lifikie malengo ya kupata takwimu sahihi.
Kunenge alitoa agizo hilo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku 21 ya Makarani wa Sensa wapatao 211 kutoka Halmashauri zote za mkoa huo.
Kunenge alisema kuwa zoezi la sensa kwa nchi ndiyo kila kitu hivyo Makarani hao wanapaswa kwenda kuwafundisha kwa usahihi Makarani wa ngazi za wilaya za mkoa huo.
"Mnapotoa mafunzo kwa Makarani mnapaswa kuzingatia taratibu na kanuni za sensa mlizofundishwa kwa usahihi na ufasaha,"alisema Kunenge.
Akizungumzia kuhusiana na kuwa wazalendo wakufunzi hao, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri alisema kuwa Makarani hao wamepewa dhamana kubwa na nchi na wajitoe kizalendo kwa ajili ya nchi yao hata kama zitatokea changamoto mbalimbali kwani zoezi likiharibika leo ni hasara kwa miaka 10 ijayo.
Msafiri alisema kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto za maendeleo kutokana na baadhi ya waliohusika na sensa zilizopita kwa kutotoa takwimu sahihi hivyo rasilimali kuonekana hazitoshelezi
Kwa upande wake mratibu wa sensa mkoa wa Pwani Adela Temba alisema kuwa Makarani hao wa sensa wote wamefaulu baada ya kufanya mitihani ambapo ufaulu ni asilimia 74.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...