WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), imesema kupitia Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar Es Salaam  mwananchi anaweza kujisajili mtandaoni ili kuweza kujaza fomu kwaajili ya kupata cheti cha kuzaliwa.

Hayo yamesemwa Afisa Mawasiliano kutoka RITA, Jafari Malema wakati akizungumza na Mwandishi wetu katika Maonesho ya Sabasaba na leo Julai mosi, 2022, amesema kuwa Mwananchi akijisajili katika mkoa wowote wa Tanzania anaweza kupata cheti chake kupitia ofisi za kanda alipo. 

"Unaweza kujisajili kupitia E-huduma  kwenye Mtandao wetu wa RITA kwa kufungua akaunti ili uweze kutuma maombi yako, kama ni ya Cheti cha Kuzaliwa, chako wewe, cha Mtoto au bodi ya wadhamini." Amesema Malima

Amesema hijalishi umezaliwa Mkoa gani unaweza kupata cheti cha kuzaliwa kieletroniki bila matatizo yeyote.

Licha ya hayo Malema amewakaribisha wananchi kwa Ujumla wale ambao hawana cheti cha Kuzaliwa wafike katika maonesho ya kibiashara ya 46 maarufu kama Sabasaba kwaajili ya kijipatia huduma mbalimbali zinazotolewa katika banda hilo. 

Amesema huduma wanazozitoa ni pamona na kutoa elimu jinsi ya kuandika wosia, kusajili vizazi na vifo na  kutoa cheti cha ndoa kwa mujibu wa sheria.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wakipata huduma katika maonesho ya Kimataifa ya kibiashara yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano waWakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafari Malema akizungmza na waandishi wa habari katika maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Kulia Msajili Mwandamizi wa (RITA) Rehema Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam. kushoto Afisa Mawasiliano wa (RITA) Jafari Malema
Muonekano wa Banda la RITA katika vinwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.




Wananchi wakipata huduma na katika maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...