Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

SERIKALI imeagiza timu zote zinazoshiriki mashindano ya Ligi Kuu na mashindano mengine, kuhakikisha wanajenga viwanja vyao vya kisasa kulingana na Sera ya Michezo ya Tanzania, Sura ya 7 inavyoelekeza.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa michezo jijini Dar es Salaam, wakati wa tukio la utoaji tuzo za ‘NBC, TFF Awards”.

“Nawaagiza Baraza la Michezo (BMT) na Shirikisho la Soka (TFF) andaeni kikao maalum cha Viongozi wote wa Vilabu, nikutane nao tujadili suala hili la kila timu kujenga uwanja wake”, amesema Mhe. Mchengerwa.

“Serikali hatupo nyuma, tutahakikisha tutakarabati viwanja mbalimbali nchini kwa kuweka Nyasi halisi na Nyasi bandia kwa mahitaji ya viwanja hivyo hapa nchini”, ameeleza.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema kuwa Tanzania ina azma ya kuandaa Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, huku kukiwa na mpango wa kuandaa Michuano kama hiyo kwa upande wa Wanawake (WAFCON) mwaka 2024.

Pia, Mhe. Mchengerwa amewakumbusha Viongozi mbalimbali wa Michezo kuzingatia Maadili ya Uongozi huku akiwakumbusha kuiga mfano kwenye Mataifa yaliendelea kwenye michezo kwa kuzingatia nidhamu na maadili katika michezo hiyo.

“Wale wanaokiuka maadili kwenye michezo, acheni mara moja, nasema acheni kabisa ili tuendeleze mchezo wetu wa mpira wa miguu hapa nyumbani”, amesema Mchengerwa.

Hata hivyo, ameahidi kuwa Serikali inaendelea na azma yake ya kujenga Ukumbi mkubwa wa kisasa utakaobeba idadi ya watu wengi, utakaojengwa eneo la Kawe, jijini Dar es Salaam, “Huenda sherehe za Tuzo kama hizi za ‘NBC TFF Awards’ tukazifanyia kwenye ukumbi huo msimu ujao.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...