Na Jane Edward, Arusha


Serikali imeanza zoezi la kuwasajili na kuwatambua wakulima nchi nzima lengo likiwa kujua wakulima walipo na aina ya kilimo wanacholima

Akizungumza wakati wa maonyesho ya kilimo biashara yaliyowashirikisha wakulima kutoka Kanda ya Kaskazini Naibu Waziri wa kilimo Antony Mavunde anasema zoezi hilo litaisaidia serikali kuwatambua wakulima na kukitambua kilimo wanachokifanya hususani wanapopatiwa ruzuku za mbolea na serikali

Amesema kuwa mara nyingi wakulima wanakuwa hawatambuliki wanalima nini na kama wamenufaika na kilimo au kama kuna changamoto ili waweze kusaidika ikiwemo kupatiwa ruzuku za mbolea.

Ameongeza baadhi ya watu wamekuwa wakinufaika kupitia mgongo wa mkulima na endapo serikali itaweza kumsaidia mkulima Kwa kufatilia kilimo anacholima.

"Miaka mitano iliyopita tulikuwa tukitoa ruzuku za mbolea lakini zilikuwa hazimfikii mkulima zinaishia kwenye mikono ya wachache na hili zoezi la kuwatambua wakulima litaenda kuondoa adha hiyo" Alisema Mavunde

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tari Daktari Geofrey Mkamilo anasema tangu kuanza kwa maomyesho hayo wakulima wamekuwa wakipatiwa elimu na matumizi sahihi ya pembejeo za kisasa na kwenda kuzitumia lengo likiwa ni kumsaidia mkulima kufanya kilimo biashara.

Amesema Kwa sasa wakulima inabidi wabadilike waachane na kilimo cha mazoea ambacho hakina tija na kujikita katika kilimo chenye tija ili kujikwamua kiuchumi.

"Achaneni na kilimo cha mazoea chukueni elimu ya pembejeo za kisasa ili muweze kupata mazao mengi yatakayo badilisha maisha ya mkulima mmoja mmoja" Alisema Mkamilo

Naye kaimu mkurugenzi wa Tari Seliani Rose Ubwe amesema kituo cha utafiti Tari Seliani kimekuwa kikitoa elimu juu ya zana za kisasa za kilimo na kuwataka wakulima kutembelea kituo hicho ili kujionea mashamba hayo na kujifunza.

Amefafanua kuwa Kituo cha Tari Seliani kimekuwa na mashamba ya mfano ya kilimo bora na kupata elimu ya matumizi sahihi ya kilimo bora.

Maonyesho haya yalianza kufanyaka mwaka 2012 ambapo wakulima na wadau wa kilimo zaidi ya mia sita wameshiriki.

Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde akisalimiana na wakulima katika maonyesho ya kilimo biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Tari Tanzania Daktari Jofrey Mkamilo akizungumzia umuhimu wa maonesho hayo.
Naibu waziri wa Kilimo Akizungumza na wakulima katika maonesho hayo.
 Mavunde akiwa katika picha na wanafunzi waliokuja kwaajili ya kujifunza masuala ya kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...