Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

WACHEZAJI Watatu wa Klabu ya Lugalo Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wameibuka washindi katika Mashindano ya wazi ya (Kilimanjaro Open 2022) yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Arusha.

Wachezaji hao ni Leticia Kapalia aliyeibuka mchezaji Bora wa Siku kwa mikwaju 139 kwa siku mbili huku Nicholus Chitanda ameibuka kinara wa kupiga Mpira umbali mrefu zaidi ya wachezaji wote.

Upande wa Wachezaji watoto (Juniors) Rahimu Ally ameibuka mshindia kwa mikwaju 81siku ya kwanza na 71 kwa siku ya Pili.

Akizungumzia ushiriki wa timu ya Lugalo Nahodha wa klabu hiyo Meja Japhet Masai amesema Lugalo itaendelea kutoa washindi kwa kila michuano itakayofanyika ndani na nje ya nchi.

Aidha Meja Masai amesema timu inarejea Dar es salaam kujiandaa na mashindano yanayokuja ili kuendelea kushikilia rekodi ya Ubingwa kila mara.

Katibu wa Mashindano kutoka (TGU) Enock Magile akikabidhi zawadi Kwa Mshindi aliefanya vizuri katika Mashindano ya (Kilimanjaro open 2022) yaliyofanyika Mkoani Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...