Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI imetenga Sh bilioni 6.4kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa ubora, kutoa mafunzo ya mapitio ya mitaala, usimamizi na uendeshaji wa vyuo vikuu.
Aidha, imeziagiza taasisi hizo kutoa kipaumbele katika mchakato wa kuja na mitaala itakayosaidia upatikanaji wa kujiajiri miongoni mwa vijana na wahitimu.
Hatua hii imekuja wakati kukiwa na wimbi la ukosefu wa wataalamu katika vyuo mbalimbali nchini.
Akizungumza leo katika kilele cha maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kuanzia Julai 18-23 mwezi huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael amesema ipo haja ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira hasa ukosefu wa wataalamu wenye uwezo.
Amebainisha kuwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Heet) ambao ni ufadhili wa Benki ya Dunia wa USD milioni 425 Serikali imetenga Sh6.4 bilioni ambazo pamoja na mambo mengine ni kwa ajili ya kuboresha mitaala ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
.
"Tunahitaji kuimarisha usimamizi wa udhibiti wa ubora ili kuiweka Elimu inayotolewa nchini kwenye ramani ya dunia ili kuepuka kutoa wataalamu kutoka nje Yaa nchi wenye fani mbalimbali," amesema.
Amesema mradi huo pia utawezesha wadhibiti ubora katika elimu kuwezeshwa na kuimarisha kazi zao, ikiwemo miundombinu ya vyuo vikuu na upanuzi wao wa vyuo vishiriki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) Prof. Penina Muhando amesema maonesho hayo yana lengo ya kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya taasisi zetu za elimu ya juu .
"Maonesho haya yatawezesha wananchi kupata fursa za kuona shughuli mbalimbali zinazotendwa na taasisi za elimu ili kuwasaidia wanaotaka kuendelea na elimu ya juu kufanya maamuzi ya kujiendeleza". Amesema Prof.Muhando.
Kwa niaba ya washiriki wa maonyesho hayo, Prof Raphael Chibunda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) amesema maonyesho hayo yamesaidia vyuo vikuu kuongeza udahili wa wanafunzi.
Maonyesho hayo ya vyuo vya elimu ya juu hufanywa kila mwaka na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambayo husaidia kurahisisha mawasiliano kati ya vyuo, wanafunzi na wazazi au walezi.
Katibu Mkuu Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza wakati wa kufunga wiki ya maonensho ya 17 ya Vyuo Vikuu yaliyokuwa yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yalianza Julai 18,2022 na yamemalizika leo Julai 23, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...