SHULE
ya Kata Zogowale iliyopo Kata ya Misugusugu, Halmashauri ya Mji Kibaha
imeendelea kung'ara kwenye ufaulu wa matokeo ya kidato cha sita,2022
yaliyotangazwa tarehe 5 Julai,2022 kwa kufaulisha kwa 100 asilimia.
Mkuu
wa shule hiyo Tatu Mwambala amesema kuwa ufaulu umekuwa wa kuridhisha
zaidi Mwaka huu, Amesema
kuwa wanafunzi 7 wamepata daraja la kwanza, 87 daraja la Pili,78 daraja
la 3 huku wanafunzi 2 wakipata daraja la nne.
Mwambala
ameongeza kuwa ingawa hakuna aliyepata daraja sifuri kati ya wanafunzi
174 lakini kimkoa imekuwa nafasi ya 31 kati ya shule 45 huku Kitaifa
ikishika nafasi ya 592.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde, ameipongeza Idara
ya Elimu Sekondari kupitia kwa Mkuu wa Idara Mwalimu Rosemary Msasi kwa
usimamizi Mzuri, Walimu, Wazazi na wanafunzi wenyewe kwa mafanikio hayo
na kwamba hii iwe Chachu zaidi kwa miaka mingine.
Aidha,Katibu
wa tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kibaha Marco Bahebe kando ya
kuwapongeza amesema mafanikio haya yametokana na nidhamu na matumizi
sahihi ya Sheria, taratibu na Kanuni.
Shule ya Sekondari Zogowale inafundisha tahasusi za HGK,HKL,CBG na PCB.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...