Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro akiangalia wa wafanyakazi RITA wanavyohudumia wananchi katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar ws Salaam kushoto ni Kabidhi Waisii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala la Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)Angela Anatory.
Kabidhi Waisii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Angela Anatory akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya kuwahudumia wananchi wanaotaka vyeti vya kuzaliwa katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*Wananchi wadai wanapata huduma bora kutoa RITA kwenye maonesho
Na Chalila Kibuda
Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro amesema kuwa Wakala wa Usajili Udhilisi na Udhamini (RITA) wanafanya kazi vizuri katika kuhumia vyeti vya kuzaliwa umati kwa wa Umati wanaotembelea maonesho ya Sabasaba
Dk.Ndumbaro amesema hayo mara baada ya kukuta umati wa wananchi katika Banda la RITA alipotembelea Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ameshuhudia umati huo wa watu alipotembelea banda la RITA, leo Julai 6, 2022 kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi ndani ya viwanja vya Sabasaba na kuongeza idadi hiyo kuwa itaendelea kuongezeka.
“Leo nimetembelea banda la RITA, ambayo ni moja ya taasisi zilizopo katika Wizara ya Katiba na Sheria, nimekuta kuna umati mkubwa wa watu. Kwa mujibu wa taarifa nilizopewa, zaidi ya watu 1,000 wanakuja kujipatia huduma zao hapa kila siku,” alifafanua Dkt. Ndumbaro.
Aliendelea kusema kuwa, asilimia kubwa ya Watanzania waliojitokeza ni kwa ajili ya usajili wa vizazi na huduma nyingine zinazotolewa na RITA. Aidha amewataka Watanzania wanaohitaji vyeti vya kuzaliwa kufika katika viwanja vya Sabasaba, banda la RITA ili waweze kupata huduma hiyo.
Dkt. Ndumbaro amewapongeza Wafanyakazi wa RITA kwa kufanya kazi bila kupumzika masaa yote na amewataka wafanyakazi hao kuendelea kuwahudumia Watanzania kama ambavyo Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan alivyowaagiza kuwahudumia Watanzania.
Kwa upande wake, Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa RITA, Angela Anatory amesema kuwa watu wengi wanajitokeza kufanya usajili katika maonesho ya Sabasaba kwa sababu wanapata huduma nyingi katika eneo moja.
“Kila ambapo tunapokuwa na matukio kama haya, Sabasaba na Nanenane tunatoa huduma, lakini pia huduma hizi zinapatikana katika ofisi kama vile Makao Makuu ya RITA, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, lakini pia kampeni kama hizi huwa tunazifanya mashuleni, na katika vituo vya afya vinavyotoa huduma ya mama na mtoto kwa ajili ya kuwasajili watoto chini ya miaka Mitano,” alifafanua Angela.
Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa huduma ya kupata vyeti vya kuzaliwa inapatikana pia kwa njia ya mtandao, ambapo muombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi ya usajili inayopatikana katika tovuti ya RITA na kuituma bila kufika ofisi za RITA.
Aidha amesema kuwa, taasisi hiyo imesajili zaidi ya Watanzania 2800 kuanzia tarehe Juni 28, 2022 yalipoanza maonesho hayo ya Sabasaba mpaka Julai 5, 2022.
Wananchi wengi waliofika katika banda la RITA kwa ajili ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa, wamefurahia huduma hiyo namna ambavyo imekuwa rahisi na ya haraka tofauti na walivyotegemea.
“Nimekuja kufanya usajili kwa ajili ya kupata cheti changu cha kuzaliwa, ili niweze kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa. Huduma ni nzuri, kwani nimefika leo na nimefanikiwa kukamilisha taratibu zote, nasubiri kufuata cheti changu baada ya siku 10,” alifafanua Joseph Osca kutoka Tegeta
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...