Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.
“Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kujua katika ramani mahali mitaa, barabara zilipo. Mmefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuja kujifunza alisema waziri”
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe George Simbachawene katika ziara aliyoifanya Kata ya Pwaga na na Luhundwa alipotembelea na kufanya Mikutano.
“Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya postikodi ili watanzania wajulikane wanakaa wapi; jambo la kuweka mitaa, lakini pia barabara na namba kwenye nyumba katika Halmashauri wilaya ya Mpwapwa na jimbo la Kibakwe limefanyika kwa mazingira makubwa”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene akizungumza na wananchi wa kata ya Pwaga na Luhundwa alipotembelea na kufanya mikutano ya hadhara katika jimbo la kibwakwe Halmashauri ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene akikagua utekelezaji wa Operesheni anwani Makazi katika Kijiji cha Mpwanila kata ya Luhundwa katika jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...