Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Mnzava Emmanuel akizungumza na wananchi (Hawapo pichani) waliotembelea banda lao katika maonesho ya biashara ya Kimataifa ya sabasaba na kuwapatia maelezo namna ya  kufanya ufugaji bora kwa kutumia mbegu ya Ng'ombe dume aina ya Borani.

 

 

KATIKA kuhakikisha juhudi za ufugaji zinakuwa na tija na endelevu, Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO imekuja na ofa kubwa kwa watanzania kwa kutoa punguzo la asilimia 14 kwa madume ya ng’ombe bora aina ya Borani kutoka kwenye bei ya awali.

Iwapo ofa hii itatumiwa na wafugaji wengi nchini utasaidia kupatikana kwa mifugo inayopata uzito katika kipindi kifupi ili ipelekwe sokoni.

Meneja masoko wa Ranchi ya Taifa, Mnzava Emmanuel ameyasema hayo leo Julai 10, 2022 katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Amesema, ofa hiyo imeanza toka kipindi cha sabasaba kilipoanza na itaisha Julai 20, 2022 ikiwa imejumuisha mpaka sikukuu ya Idd huku wakisubiri kuingia kwenye maandalizi ya ofa mpya kwa ajili ya Nanenane.

Amesema mbegu hiyo aina ya Borani ni ng’ombe dume ambayo mfugaji anaweza kupandisha kwa Ng’ombe jike wa kienyeji .

Ametanabaisha kuwa Viwanda vya mifugo vipo vingi lakini vinakosa mifugo kwa sababu wafugaji hufuga chini ya kiwango.

"Tangu kuanza kwa maonyesho haya, muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa , wananchi wengi wenye makundi ya mifugo wamekuwa wakifika katika banda letu kwa ajili ya kununua Ng'ombe hawa wa Borani na wengine ambao hawakuweza kufika basi wamekuwa wakipiga simu na kupatiwa control namba kisha wanaenda kwenye ranchi wanalipa fedha na kuchukua madume yao ". Amesema Emmanuel

Amesema, wakishachukua  madume hayo ya mbegu wanaenda kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kwenda kupandisha katika makundi ya mifugo yao kwani unaweza ukatumia dume hilo la Borani kupandisha kwa majike ya asili na matokeo yake ni kwamba utapata machotara wa N'gombe wanaokuwa kwa haraka na kwa muda mfupi huku akiwa ameishakuwa na uzito mkubwa tayari kwa kumpeleka sokoni.

Amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na mifugo inayopata uzito mkubwa kwa kipindi kifupi ili wapeleke sokoni.

Amesema, kama wafugaji watatumia fursa hii ya mbegu hizi, basi watapata mifugo ambayo itakuwa ndani ya muda mfupi kutokana na ubora wa mbegu hizo kusudi ndani ya muda huo mfupi wapeleke mifugo yao viwandani ili viwanda viweze kufanya kazi kwa uwezo wao wa kuzalisha bila kukosa raw material.

"Tunasisitiza ufugaji wa kisasa na wa kibiashara siyo kukaa na ng'ombe  miaka sita hadi saba, ukitumia mbegu hii miaka miwili tu ng'ombe anakuwa ameishafikia uzito wa kilo 400 unampeleka sokoni," amesema

Ameongeza kuwa pia kuna fursa za uwekezaji ambapo wametenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji mkubwa wa viwanda vya kuchinja ng'ombe, maziwa, malisho, mgozi,  kuchakata nyama, na viwanda vya mazao ya ngozi kama vile mikanda makoti mabegi nk.

"Maeneo haya yapo kwa wawekezaji wa kimkakati, kama yupo mtanzania ambaye anafikiri anaweza kuwekeza kimkakati na mradi wake ukaleta matokeo makubwa na faida kwa wananchi wengi maeneo ya kuwekeza viwanda hivyo kwenye huo mnyororo mzima wa thamani yanapatikana na tumetenga tayari kwenye ranchi zetu za Taifa 14 ambapo katika kila kanda kunaranchi moja ama mbili,” amesema Emmanuel 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...