Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KIUNGO Mshambuliaji wa Tanzania, Abdul Suleiman Sopu amekamilisha usajili katika Klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam akitokea Klabu ya Coastal Union FC ya Tanga.
Azam FC ikiwa chini ya Mmiliki wake Yusuf Bakhresa imekamilisha usajili wa Mchezaji huyo aliyewatesa Yanga SC na kupiga ‘Hat-Trick’ katika mchezo wa Fainali ya Michuano ya Kombe la ASFC, mchezo uliopigwa jijini Arusha kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid.
Azam FC wameamua kuvunja kibubu kujiandaa na msimu ujao wa mashindano, sajili za matajiri hao wa Chamazi zinasimamiwa na Mmiliki wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa akiwa sanjari na Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Abdulkarim Amin Popat.
Hadi sasa, Azam FC wamekamilisha usajili wa Abdul Suleiman Sopu, Isa Ndala, Tape Edinho, Kipre Junior, Cleophace Mkandala, Kocha wa Makipa, Dani Cadena na Kocha wa Washambuliaji, Kali Ongala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...