Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road (ORCI) Dk.Julius Mwaisalage akiwa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati alipotembelea Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa , Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakipata elimu na huduma katika Banda la Taasisi ya Ocean Road maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa , Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKURUGENZI Mtendaji wa Wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dk.Julius Mwaisalage amesema kuwa katika siku za usoni taasisi bobevu ya kuhudumia wagonjwa wa Satani katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dk.Mwaisalage ameyasema hayo leo katika Banda la Taasisi ya Ocean Road (ORCI) wakati alipotembelea Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika maonesho hayo wameshiriki katika kutoa elimu ya saratani kutokana na ugonjwa huo kuongezeka ambapo watapima watu ndani ya maonesho Saratani za Matiti , Shingo ya Kizazi pamoja na Tezi Dume kwa Wanaume.
Dk.Mwaisalage amesema kuwa wanatarajia kuanza huduma za upasuaji katika Taasisi hiyo kutokana na Rais Samia Hassan Suluhu kuendelea kutoa fedha katika miradi mbalimbali ya kuhakikisha wananchi wanapata hudumu bora za saratani.
Amesema katika maonesho hayo wataalam watatoa elimu juu ya visababishi vya saratani mbalimbali pamoja na hatua za kuchua katika kukabiliana nazo pamoja na wanaogundulika kuanza kupata huduma bure huku watu wenye Ualbino kupata mafuta bure.
Amesema kuhusu tiba ya mtandao wanasubiri Shirika la Mawasiliano Tanzania wafunge mkongo wa Taifa ambapo watatoa huduma ya mtandao nchi zima kwa kila mgonjwa alipo atahudumiwa kuangalia picha akiwa na madaktari wa hospitali husika.
Amesema kuwa katika kuhakikisha Dawa za Saratani zinaatikana Rais Samia Hassan Suluhu alitoa sh.Bilioni pamoja na kutoa Sh.Bilioni 18 kwa ajili ya mashine ya MRI ambapo mradi huo kufikia Septemba utakuwa umekamilika.
Amesema katika maonesho hayo wanatoa chanjo ya Homa ya Ini pamoja na UVIKO 19 lengo ni kuakisi kauli mbiu ya Maonesho ya Tanzania ni mahala salama pa Uwekezaji na Biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...